Featured Kitaifa

WAZIRI SIMBACHAWENE ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA RAIS,MIPANGO NA UWEKEZAJI MAONESHO WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Written by mzalendo

WAZIRI  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene,akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Idara ya Uwekezaji Sekta Binafsi Bw.Aristides Mbwasi mara baada ya kutembelea Banda la Ofisi ya Rais,Mipango na Uwekezaji wakati wa Maonesho  ya Wiki ya Utumishi  wa Umma yanayofanyika  katika Viwanja vya Chinangali  jijini Dodoma.

WAZIRI  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene,akifurahia jambo na  Mkurugenzi Idara ya Uwekezaji Sekta Binafsi Bw.Aristides Mbwasi  baada ya kupata maelezo katika  Banda la Ofisi ya Rais,Mipango na Uwekezaji wakati wa Maonesho  ya Wiki ya Utumishi  wa Umma yanayofanyika  katika Viwanja vya Chinangali  jijini Dodoma.

 

Viongozi mbalimbali wa Serikali wametembelea Banda la Ofisi ya Rais,Mipango na Uwekezaji kwenye maonesho ya  Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo yanafanyika kitaifa jijini  Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 23 June, 2024.

Miongoni mwa viongozi waliotembelea ni Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene.

About the author

mzalendo