Na Alex Sonna-DODOMA
TANZANIA imeshindwa kutamba nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Sudan katika mchezo wa kirafiki wa Kimataifa uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Sudan walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya pili likifungwa na Sadiq Totto baada ya kipa Metacha Mnata kuutema mpira hadi mapumziko wageni walienda wakiwa na bao hilo moja.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko na katika dakika ya 67 Simon Msuva aliisawazishia Taifa Stars akimalizia pasi ya George Mpole.
Mchezo huu ulikuwa wa pili kwa Tanzania baada ya mchezo wa kwanza kucheza na Afrika ya Kati na Stars kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.