Featured Michezo

NYOTA WA ARSENAL AIPELEKA GHANA KOMBE LA DUNIA 2022

Written by mzalendoeditor

TIMU ya Ghana ‘Black Stars’ imekuwa Taifa la kwanza kufuzu Michuano ya Kombe la Dunia litakalofanyika nchini Qatar 2022 baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na Nigeria mchezo uliopigwa uwanja wa Abuja nchini Nigeria.

shujaa wa Ghana ni kiungo mkabaji wa Arsenal Thomas Partey alifunga bao dakika ya 10 ya mchezo kabla ya wenyeji kusawazisha kwa mkwaju wa Penalti ikifungwa na William Troost -Ekong.

Kwa sare hiyo Black Stars wanakwenda nchini Qatar kwa bao la ugenini.

About the author

mzalendoeditor