Featured Kitaifa

WATOA HUDUMA WA AFYA WAJENGEWA UWEZO MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

Written by mzalendoeditor

Na. Majid Abdulkarim, WAF -DODOMA
Serikali kupitia Wizara ya Afya imekuja na mkakati wa kuwajengea uwezo wataalamu waliopo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ya msingi nchini ili waweze kutoa matibabu sahihi kwa wagonjwa wa magonjwa yasiyo yakuambukiza.
Kauli hiyo imebainishwa Jijini Dodoma na Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasiyo yakuambukiza kutoka Wizara ya Afya, Dkt. James Kiologwe wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya wataalamu wa afya kutoka mikoa nane nchini ambapo amesema kuwa mkakati wa serikali ni kuvifikia vituo 500 vya afya ifikapo 2023
Dkt. Kiologwe amesema kupatikana kwa huduma hizi katika ngazi ya msingi kutaendana na upatikanaji wa vifaa tiba vya kuchunguza na kutibu magonjwa hayo ili kuwapunguzia gharama wananchi kwa kutumia fedha nyingi  za kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizi na badala yake zitapatikana katika maeneo waliopo.
“Takwimu zinaonyesha kwamba asilimia zaidi ya 70 ya wagonjwa wenye tatizo la shinikizo la juu la damu hawajijui hali zao na zaidi ya theluthi mbili hawapo katika matibabu hivyo hivyo na kwa upande wa kisukari”, ameeleza Dkt. Kiologwe.
Dkt. Kiologwe amesema kuwa Tafiti zinaonyesha kuwa uwezo wa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi  bado havina uwezo wa  kutoa huduma hizo hivyo Serikali imekuja na mkakati huo  wa kutoa huduma hizo ambapo ndo wananchi wengi wanapatikana
Hata hivyo Dkt. Kiologwe amesema kuwa magonjwa yasiyo yakuambukiza yamekuwa yakiongezeka nchini takribani watu 26 kati ya watu 100 wana tatizo la shinikizo la juu la damu na watu 10 kati ya 100 wana tatizo la kisukari na visa vipya vya saratani takribani 40,000 kwa mwaka.
Pia Dkt. Kiologwe ameendelea kusema kuwa watu 8,000 wanahitaji huduma za usafishaji wa damu kutokana na changamoto ya figo na hii inatokana na madhara yatokanayo na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama shinikizo la juu la damu, Saratani na Kisukari.
Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Chama cha Kisukari Tanzania, Waziri Ndonde amesema  kuwa wataalamu hao wakishajengewa uwezo watakuwa na jukumu kubwa la kwenda kufundisha watalamu wenzao katika maeneo yao ili kuwa na watalamu wenge katika ngazi ya msingi wenye uelewa juu ya magonjwa haya yasiyo yakuambukiza.
“Nitoe wito kwa wataalamu walopatiwa mafunzo haya juu ya magonjwa yasiyo yakuambukiza kuwa ujuzi huu ukatumike katika kunufaisha jamii ya watanzania inayowazunguka katika maeneo yao ili kupunguza changamoto za wananchi kusafiri mwendo mrefu kufuata huduma hizi na kutumia gharama nyingi”

About the author

mzalendoeditor