Featured Kimataifa

AJALI YA NDEGE CHINA : ABIRIA 132 WAFARIKI, HAKUNA MANUSURA

Written by mzalendoeditor

IMG_20220327_143955

Abiria wote 132 walikuwa kwenye Ndege ya Chinese Eastern Airlines aina ya Boeing 737 wamethibitishwa kufa baada ya ndege hiyo kuanguka.

Mamlaka ya anga ya China CAAC imethibitisha hilo jana Jumamosi Machi 26, 2022 ambapo Naibu mkurugenzi wa CAAC Hu Zhenjiang amewaambia waandishi wa habari kwamba hakuna dalili yoyote ya manusura kwenye eneo la ajali lililoko katikati ya msitu mkubwa katika eneo la Guangxi karibu na jiji la Wuzhou.

Abiria 120 walitambuliwa kupitia vipimo vya vinasaba wakati familia za wahanga zikiwa zinasubiri kwa siku kadhaa kusikia taarifa za ndugu zao kuokoloewa na vikosi vya uokozi.

Mamlaka bado ziko njia panda katika kung’amua chanzo cha ajali hiyo ambayo ni mbaya zaidi kutokea nchini China katika kipindi cha karibu miaka 30.

Ndege ya shirika la China Eastern, namba MU5735, iliyokuwa imebeba abiria 123 na wafanyakazi wake 9 ilianguka katika sehemu ya milima jimbo la Tengxian, Guangxi mnamo Machi 21, 2022.

About the author

mzalendoeditor