Jeshi la Polisi Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara, limewataka wanafunzi shule za msingi na sekondari wilayani humo kuwa makini na misaada wanayopewa ikiwemo usafiri na chakula kwasababu watu wenye niambaya huitumia kuwafanyia uhalifu.
Maneno hayo yametolewa na Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Babati (Central Babati), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Amiri Mlemba, Machi 25, 2024, wakati akitoa elimu ya usalama na uraia kwa wanafunzi wa shule ya msingi Bagara, Kata ya Bagara, Halmashauri ya Mji Babati Mkoani Manyara
Amewataka wanafunzi hao kushirikiana na walimu pamoja na wazazi katika kupashana habari za kubaini na kutanzua uhalifu katika jamii hususani ukatili wa kingono kwa watoto wadogo kwani bila kupashana habari uthibiti wake utakuwa mgumu