Featured Kitaifa

TUMIENI VIJIWE VYA KAHAWA KUIMARISHA USALAMA – INSP MLAGALA

Written by mzalendo

Polisi Kata wa Mganza wilayani Uvinza, Mkoa wa Kigoma amewataka wananchi wa Kata hiyo kutumia vijiwe vya kahawa maarufu kwa jina la meza ya duara mkoani humo kujadili masuala ya kiusalama ndani ya maeneo yao hususani namna watakavyoshiriki kubaini na kuzuia uhalifu.

Hayo yamesemwa Machi 23,2024 na Mkaguzi msaidizi wa Polisi (A/INSP) Frank Mlagala Polisi kata wa kata hiyo wakati akitoa elimu ya usalama wetu kwanza ambapo amewataka wananchi hao katika mijadala wanayojadili wajadili masuala ya kuimarisha ulinzi na usalama wa kata hiyo kupitia ulinzi jirani na vikundi vya ulinzi shirikishi.

Polisi kata Mlagala amesema vijiwe hivi hutumika kujadili mambo mbalimbali ya kisiasa na michezo ni vyema pia vikatumika kujadili masuala ya kuimarisha usalama wa kata hiyo.

Pamoja na hayo amewataka wananchi hao kuendelea kutii sheria bila shurti na kutokujihusisha na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi.

Kwa upande wao wananchi wameahidi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kubaini na kuzuia uhalifu.

About the author

mzalendo