Featured Kitaifa

DIT COMPANY KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA SOLUTION PLUS YAENDESHA MAFUNZO JUU YA MATUMIZI YA NISHATI YA UMEME KWA VYOMBO VYA MOTO

Written by mzalendoeditor

 

Kampuni Tanzu ya Taasisi ya Teknolojia Dar-es-salaam (DIT Company) kwa kushirikiana na Kampuni ya Solution Plus yaendesha mafunzo ya siku moja juu ya Matumizi ya nishati ya Umeme kwenye Vyombo vya Moto.

Mafunzo haya yanalenga kupata idadi kubwa ya baskeli za umeme na bajaji katika jiji la Dar es Salaam ambazo zinatumika kusambaza vifurushi badala wya kutegemea pikipiki pekee.

Mafunzo haya yamelenga kuangalia mafanikio na changamoto wanazokutana nazo watumiaji wa baskeli hizi maarufu kwa jina la Fasta ambao wamekuwa wakizitumia mara kufunga mfumo wa umeme na kujadiliana njia bora ya kutatua changamoto hizo ili kuweza kuongeza idadi ya baskeli hizo kutoka 16 zilizopo sasa

Emilie Martin mtafiti mwandamizi kutoka solution plus ameishukuri DIT Company kwa kushirikiana nao katika kuwezesha mradi huu unaofadhiliwa na EU

“Naishuruku DIT Company kwa ushirikiano katika kuwezesha programu hii kufanyika kwa awamu ya kwanza, kuwezesha uunganishani wa baskeli pia kuhakikisha watumiaji kutoka fasta wanamahali salama pa kuchaji na kulaza hizi baskeli” alisema Emilie.

Mradi huu umekuwa kivutio kwa miji mingine kama Nairobi na kufanya watamani kujifunza kupitia Tanzania.

Nae kiongozi wa Fasta Filbert Mbecha ameishukuru DIT kwa kuwawezesha kutumia baskeli hizi kwa uhakika wakati wote walipohitaji kuzotumia “Kampuni ya DIT imekuwa msaada sana katika kuendesha mradi huu kwa kuhakikisha zinakuwa salama na kuwezesha kupata umeme ili waweze kuzitumi:

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Kampini Tanzu ya DIT ameishukuru Solution Plus kwa ushirikiano huu ambao umewezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo katika kuziunganisha baskeli hizi na kutengeneza bajaji za umeme.

Mradi huu uliofadhiliwa na Umoja wa Ulaya unatekelezwa katika miji miwili Afrika yaani Dar es Salaam Tanzania na Kigali Rwanda pekee.

About the author

mzalendoeditor