Featured Kitaifa

MIGODI YA BARRICK BULYANHULU NA NORTH MARA ILIVYOSHEREKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Written by mzalendoeditor
Wafanyakazi Wanawake wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu kabla ya kushiriki kutoa misaada katika kituo cha afya Bugarama

Wafanyakazi Wanawake wa Barrick North Mara wakiandamana kuadhimisha siku yao.
Meneja Mkuu wa Barrick North Mara,Apolinary Lyambiko akitoa cheti kwa mmoja wa wafanyakazi wa mgodi huo wakati wa maadhimishi ya Siku ya Wanawake Duniani.
Baadhi ya wafanyakazi wanawake wa North Mara wakiserebuka kuadhimisha siku yao.
Baadhi ya wafanyakazi wanawake wa Barrick North Mara wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaopata malezi katika kituo cha City of Hope wilayani Tarime
Wafanyakazi Wanawake wa mgodi wa Barrick Bulyanhulu kabla ya kushiriki kutoa misaada katika kituo cha afya Bugarama
Wafanyakazi Wanawake wa Barrick Bulyanhulu katika picha ya pamoja baada ya kutoa msaada katika kituo cha afya cha Bugarama.
Baadhi ya wawakilishi wa Wafanyakazi Wanawake wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu wakikata keki katika sherehe ya kuadhimisha siku yao.
Mwakilishi wa Meneja Mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu,Victor Lule akitoa cheti kwa mmoja wa wafanyakazi wanawake wa mgodi huo.Watumishi Wanawake wenye kipindi cha muda mrefu kwenye kazi na wanaofanya kazi kwa umahiri walitunukiwa vyeti.
 
***
Katika kuadhimisha siku ya Wanawake Dunia, Wafanyakazi Wanawake wa migodi ya Barrick Bulyanhulu na North Mara, wameshiriki kufanya matendo ya huruma kwa jamii ambapo Bulyanhulu wametoa zawadi mbalimbali kwa wanawake wote waliojifungua, pamoja na waliolazwa katika vituo vya afya vya Bugarama na Lunguya wakati North Mara wametoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha kulea watoto cha City of Hope kilichopo kijiji cha Ntagacha wilayani Tarime.
 
 
Pia wanawake waliodumu kwa muda mrefu katika migodi hiyo na wanaotekeleza majukumu yao kwa ufanisi wametunukiwa vyeti na kupewa zawadi,siku hiyo wanawake wamepewa semina za kuwajengea uwezo sambamba na burudani katika kusherekea siku hiyo ya kimataifa.

About the author

mzalendoeditor