Featured Kitaifa

KAMATI YA LAAC YAKAGUA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA LA HALMASHAURI YA MAGU

Written by mzalendoeditor

Kamati ya Bunge ya LAAc imekagua ujenzi wa ofisi ya Utawala ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu na kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa mradi, Kaimu Mwenyekiti Mhe. Aloyce Akwezi (Mb) ameipongeza Halmashauri kwa jengo imara litakalowafikishia huduma wananchi kwa karibu.

Pia amewataka TAMISEMI kuhakikisha inaleta fedha zilizobaki ili kuweza kukamilisha mradi uliochukua zaidi ya miaka kumi.

Wakati huo huo, Naibu Waziri (TAMISEMI) Mhe. Dkt Festo Dugange amewahakikishia kamati kuwa amepokea maelekezo ya kuleta fedha kwa mradi huo uliogharimu takribani bil 7 na utaisha kwa wakati.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa Ndg. Ngusa Samike amepokea salamu za pongezi na kusema ushirikiano wa viongozi wa Mkoa umeweza kuleta mafanikio. Kukosekana kwa migogoro ndio kumeleta mafanikio makubwa Halmashauri ya Magu.

About the author

mzalendoeditor