Featured Kitaifa

AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA SABA

Written by mzalendoeditor

images%20(15)

Mahakama ya Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa, imemhukumu mkazi wa Kijiji cha Kitelewasi, Godi Waya (30) kifungo cha maisha baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti mtoto wa miaka saba (jina linahifadhiwa).

Godi ambaye aliajiriwa kulisha ng’ombe wa bibi wa mtoto huyo alidaiwa kumtoa mwathirika chumbani kwake na kumpeleka chumba anacholala na kuanza kumbaka huku akiwa amemziba mdomo na kumtisha asimwambie mtu alichofanyiwa.

Hakimu Mkazi Edward Uphoro alikataa utetezi wa mshtakiwa huyo kuwa alibambikiwa kesi hiyo. Amesema kulikuwa na ushahidi wa kutosha kuwa yeye ndiye aliyefanya kitendo hicho na mwathirika alionekana akitoka chumbani kwake akiwa uchi.

“Suala la kubambikiwa kesi halina mashiko kwa sababu kuna ushahidi wa kimazingira na mshtakiwa mwenyewe alikiri mahakamani kuwa mtoto huyo alitoka chumani na kwamba alikuwa na mazoea ya kuingia chumani kwake. Swali ni je, kwa nini alitoka akiwa uchi?

“Mahakama hii imejiridhisha kuwa ushahidi uliotolewa na mwathirika pamoja na bibi yake ulikuwa na uzito wa kumtia mtuhumiwa hatiani kwa kosa la kulawiti,” amesema

Hakimu huyo amesema mahakama inatoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye matamanio kama hayo kwani vitendo hivyo vimekithiri katika jamii na kusababisha watoto kuishi kwa wasiwasi katika mazingira yanayowazunguka.

Source: Mwananchi 

About the author

mzalendoeditor