Mwenyekiti wa Kamati hiyoziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Naghenjwa Kaboyoka katikati akizungumza wakati wa ziara yao kwenye kituo cha Kuzalisha Umeme Hale |
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), Athanasius Nangali akizungumza wakati wa ziara hiyo |
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), Athanasius Nangali kulia akisisitiza jambo kwa kamati hiyo |
NA OSCAR ASSENGA,KOROGWE.
SHIRIKA
la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) limesema maandalizi ya utekelezaji
wa mpango mkubwa wa ukarabati wa kituo cha kuzalisha umeme cha Hale
kilichojengwa miaka 58 iliyopita yameelezwa kuwa katika hatua ya juu.
Hayo
yalibainishwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ugavi wa
Umeme Tanzania (TANESCO), Athanasius Nangali wakati wa ziara ya Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwa taratibu zote za
manunuzi ziko katika hatua nzuri.
Alisema kuwa mpango huo wa
ukarabati unalenga kuleta mabadiliko kukifanya kituo hicho kuwa cha
kisasa kinachotumia technologia ya kisasa.
Aidha alisema kituo
hicho kilijengwa mwaka 1964 na sasa hivi kinazalisha chini ya megawati
10 kati ya uwezo wake wa kuzalisha megawati 21 huku ikielezwa kuwa ni
turnine moja tu inayofanya kazi kwa sasa kati ya turnine mbili zilizopo
hapo.
Nangali alisema katika ziara ya Kamati hiyo ya Mahesabu ya
Serikali ilikuwa muhimu sana kwa mpango wa kampuni wa kutekeleza mradi
wa kufufua mtambo huo ili ufanye kazi kwa uwezo wake wote.
Awali
akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Naghenjwa
Kaboyoka alisema kamati imeona na kujiridhisha juu ya umuhimu wa
ukarabati mkubwa na mtambo wa kisasa.
Alisema ziara yao inalenga kujiridhisha iwapo gharama za mradi zinazopendekezwa zilikidhi vigezo vya thamani ya fedha.
βTumeona
haja ya kugeuza mtambo huo kuwa mtambo wa kisasa wa kuzalisha umeme
kwani bado kuna masuala ya fedha hayajakamilika na tumewaita Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la
Umeme na Afisa Mtendaji Mkuu kwenda Dodoma ili kujibu baadhi ya maswali
yaliyoulizwa na kamati,β Alisema.