Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ngurah Rai Bali nchini Indonesia leo Machi 21, 2022, kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 144 wa Umoja wa Mabunge Duniani ambapo anatarajia kulihutubia Bunge la Umoja huo kesho tarehe 22 Machi, 2022 saa 4 asubuhi katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Bali
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Mhe. Dkt. Ramadhani Dau wakati alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ngurah Rai Bali nchini Indonesia leo Machi 21, 2022, kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 144 wa Umoja wa Mabunge Duniani ambapo anatarajia kulihutubia Bunge la Umoja huo kesho tarehe 22 Machi, 2022 saa 4 asubuhi katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Bali
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akishiriki katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa 144 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na kusikiliza mawasilisho ya Maspika washiriki juu ya dhima inayohusu uhamasishaji wa Mabunge katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi leo Machi 21, 2022 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Bali nchini Indonesia. Pia Mhe. Spika anatarajia kulihutubia Bunge la Umoja huo kesho tarehe 22 Machi, 2022 saa 4 asubuhi katika Kituo hicho, kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Mhe. Dkt. Ramadhani Dau na Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Tanzania ambao ni Wajumbe wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Joseph Mhagama