Featured Kitaifa

MWENYETI TCCIA DODOMA AIOMBA TAKUKURU KUCHUNGUZA UFISADI OFISINI KWAKE

Written by mzalendo

MWENYEKITI wa Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Dodoma Khamis Fungameza,akionesha baadhi ya nyaraka kwa  Waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu upigaji wa fedha za mradi wao wa vibanda na maegesho ya magari.

MWENYEKITI wa Chemba ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Dodoma Khamis Fungameza,akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu upigaji wa fedha za mradi wao wa vibanda na maegesho ya magari.

 

MWENYEKITI wa Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Dodoma Khamis Fungameza,akifafanua jambo kwa   Waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu upigaji wa fedha za mradi wao wa vibanda na maegesho ya magari.

MWENYEKITI wa Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Dodoma Khamis Fungameza,akionesha baadhi ya nyaraka kwa  Waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu upigaji wa fedha za mradi wao wa vibanda na maegesho ya magari.

…………..

Na.Alex Sonna-DODOMA

 CHEMBA  ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Dodoma imeiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi upigaji wa mamilioni ya fedha za mradi wao wa vibanda na maegesho ya magari.

Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa  Chemba ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) mkoa wa Dodoma Khamis Fungameza,wakati  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu upigaji wa fedha za mradi huo unaofanywa na baadhi ya watu ambao hakutaja majina yao.

Amesema, mradi huo wa vibanda na maegesho ya magari ulopo eneo la Kizota jijini hapa ni mali ya TCCIA mkoa lakini hivi sasa baadhi ya watu wamejimilikisha na kukusanya mapato na kujinufaisha wenyewe.

“Mradi huu hivi sasa sisi TCCIA, hatupati kitu lakini pia serikali inapoteza mapato kwani watu hawa hawalipi kabisa kodi ya serikali naviomba vyombo kama TAKUKURU, mkuu wa mkoa watusaidia ili mradi huu urudi kwetu kwani hivi sasa watu wachache ndiyo wananufaika nao”alisema Bw.Fungameza

Pia ameeleza kuwa kwa mujibu wa vitabu vya mahesabu vinaonyesha watu hao wamekuwa wakikusanya zaidi ya Sh. milioni 90 kwenye vibanda pekee kwa mwaka.

“Vibanda tuu wanakusanya zaidi ya Sh. milioni 90 kwa mwaka pesa zote hizi wanagawana bila TCCIA kupata hata shilingi hivyo tunaomba uchunguzi ufanyike ili sisi kupata haki yetu lakini pia serikali kupata mapato yake”amesema

Aidha amesema kuwa  moja ya sababu ambazo zinachangia TCCIA kushindwa kunufaisha wanachama wake ni viongozi wengi kuwa na maslahi yao binafsi.  

“Pamoaja na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kuzunguka na Rais wa TCCIA, maeneo mbalimbali kwenda kusaini mikataba ya uwekezaji lakini sisi hatuwezi kufanikiwa kutokana na viongozi tulio nao wengi wao hawajaingia kwa ajili ya kutumikia wanachama wetu bali kwa maslahi yao binafsi.”amesema Bw.Fungameza

Hata hivyo amesema kuwa umoja kwa wafanyabishara ndiyo silaha kubwa lakini wao wamekuwa na migogoro ya muda mrefu ambayo haina tija kwa maendeleo ya sekta hiyo.

“Hivi sasa nchini kwetu mitaji kwa wafanyabiashara imekuwa kilio cha wengi lakini ukiomba mkopo benki unaupata baada ya miezi hata mitatu lakini wenzetu nchi kama China unaomba asubuhi mchana unaingia na hakuna masharti  magumu kama hapa hivyo hatuwezi kufanikiwa kabisa kuwa kama wengine”amesema

VIDEO NZIMA ANGALIA HAPA.

About the author

mzalendo