Featured Kitaifa

RAIS SAMIA ATAKA MAJAJI NA MAHAKIMU KUISHI KATIKA MISINGI YA VIAPO VYAO

Written by mzalendo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na wageni mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini ambayo Kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma tarehe 01 Februari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini ambayo Kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma tarehe 01 Februari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini ambayo Kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma tarehe 01 Februari, 2024.
Kwaya ya Mahakama ikitumbuiza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini ambayo Kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma tarehe 01 Februari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini ambayo Kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma tarehe 01 Februari, 2024.

Na.Alex Sonna-DODOMA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan,amesema Serikali itaendelea kuchukua  hatua za kuimarisha utendaji kazi wa Mahakama ikiwemo  matumizi  ya Tehama huku akiwataka Majaji na Mahakimu kuishi katika misingi ya viapo vyao kwa  kutenda haki kwa wote.

Rais Samia ameyasema hayo leo Februari 1,2024 jijini Dodoma  wakati wa kilele cha Maadhimisho ya wiki ya sheria nchini inayobebwa na kaulimbiu isemayo umuhimu wa Dhana ya haki Kwa ustawi  wa Taifa na nafasi ya Mahakama na wadau katika kuboresha mfumo jumuishi wa haki.

Amewataka Mahakimu na Majaji nchini kutoa hukumu za kesi wanazozisimamia kwa kuzingatia haki ili kukomesha malalamiko ya wananchi kutumikia adhabu ambazo siyo zao.

“Kutoa haki ni kazi ya Mungu ukitoa kwa dhuruma umetenda dhambi na dhambi ni aibu kwa mujibu wa vitabu vitakatifu ni aibu”amesema Mhe.Rais Samia

Aidha Rais Samia ameitaka Mahakama kuona Umuhimu wa kuimarisha haki madai kutokana na kuwepo kwa malalamiko  toka kwa Wananchi na kupelekea  kucheleweshwa kwa kesi.

“Jitihada kubwa zimefanyika hasa katika eneo la haki jinai hivyo ipo haja ya kuongeza jitihada katika eneo la haki madai na  kuna malalamiko kesi zinacheleweshwa mzunguko ni mkubwa wanasema inachukua hadi miezi 12 kwa shauri lililopo kwenye mahakama ya wilaya na mahakama ya hakimu mkazi kuskilizwa hadi kuhitimishwa.”

Hata hivyo Rais Samia amesema ipo haja ya kuangalia namna ya bora ya kuanza kutumia usuluhishi katika mashauri mbalimbali badala ya watu kwenda mahakamani.

“Twente kwenye usuluhishi ambao ni njia nzuri kila mmoja anatoka na amani na hauachi makovu kwa wahusika tofauti na ilivyo mahakamani ambako mashauri yanatumia muda mrefu kutolewa maamuzi na shughuli nyingine zinasimama”amesema 

Aidha ameiagiza Wizara ya Katiba na Sheria kushirikiana na wadau wa usuluhishi ili kusaidia kuudwa kwa sera ya masula yanayohusu usuluhishi.

Kwa upande wake  Jaji Mkuu wa Tanzania,Prof Ibrahim Hamis  Juma amesema kuwa mwelekeo wa utoaji wa haki nchini unaenda sambamba na Matumizi ya mifumo ya TEHAMA.

“Ushirikiano baina ya taasisi za haki jinai ni jambo muhimu sana kwa mafano mahakama tumepiga hatua kubwa sana katika maboresho kitengo chetu cha maboresho kipo tayrai kuwasaidia wadau ambao wanataka kujinza maboresho, kitengo chetu cha TEHAMA kimejijengea uwezo mkubwa wa kuweza kutengeneza mifumo inayokidhi mahitaji ya Tanzania.”amesema

Awali  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt.Elieza Fereshi amesema kuwa tayari Sheria 256 zimeshatafsiriwa kwa Kiswahili ambapo Watatumia Mfumo wa haki jinai ili kuongeza ufanisi wa kazi kwa kundi  la mawakili 

About the author

mzalendo