Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa kuboresha huduma kwa wateja na mawasiliano bora kuanzia ngazi ya awali kwa mteja uliowahusisha Madaktari na wauguzi Tanzania Bara na Zanzibar leo Januari 10,2024 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe (hayupo pichani),wakati akifungua Mkutano wa kuboresha huduma kwa wateja na mawasiliano bora kuanzia ngazi ya awali kwa mteja uliowahusisha Madaktari na wauguzi Tanzania Bara na Zanzibar leo Januari 10,2024 jijini Dodoma.
Mtaalamu wa Ubora wa Huduma kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) Bi.Shally Zumba Mwashemele,akizungumza wakati wa Mkutano wa kuboresha huduma kwa wateja na mawasiliano bora kuanzia ngazi ya awali kwa mteja uliowahusisha Madaktari na wauguzi Tanzania Bara na Zanzibar leo Januari 10,2024 jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka Wizara ya Afya Dkt.Saturini Manangwa ,akizungumza wakati wa Mkutano wa kuboresha huduma kwa wateja na mawasiliano bora kuanzia ngazi ya awali kwa mteja uliowahusisha Madaktari na wauguzi Tanzania Bara na Zanzibar leo Januari 10,2024 jijini Dodoma.
Msajili wa Baraza la Madaktari Dkt. David Poul,akizungumza wakati wa Mkutano wa kuboresha huduma kwa wateja na mawasiliano bora kuanzia ngazi ya awali kwa mteja uliowahusisha Madaktari na wauguzi Tanzania Bara na Zanzibar leo Januari 10,2024 jijini Dodoma.
Msajili wa Baraza la Wauguzi,Bi.Agness Mtawa,akizungumza wakati wa Mkutano wa kuboresha huduma kwa wateja na mawasiliano bora kuanzia ngazi ya awali kwa mteja uliowahusisha Madaktari na wauguzi Tanzania Bara na Zanzibar leo Januari 10,2024 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano wa kuboresha huduma kwa wateja na mawasiliano bora kuanzia ngazi ya awali kwa mteja uliowahusisha Madaktari na wauguzi Tanzania Bara na Zanzibar leo Januari 10,2024 jijini Dodoma.
Na.Nestory James-DODOMA
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imesema itajikita katika ubora wa huduma kwa Wateja kwa manufaa ya wananchi huku ikiwataka watumishi wa afya kuzingatia maadili ya kazi zao.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe ameyasema hayo leo Januari 10,2024 Jijini Dodoma,wakati wa Mkutano wa kuboresha huduma kwa wateja na mawasiliano bora kuanzia ngazi ya awali kwa mteja uliowahusisha Madaktari na wauguzi Tanzania Bara na Zanzibar.
Maghembe amesema kuwa Sekta ya afya ni sekta ambayo inagusa Maisha ya watu hivyo maboresho makubwa yamefanywa na Rais katika sektaya afya hivyo ni muhimu watumishi wa sekta ya afya kubadilisha mitazamo yao katika kufanya ubora wa huduma kwa wateja.
“Napenda tu niwahakikishie watanzania kuwa maboresho makubwa yaliyofanyika yataenda sambamba na utoaji wa huduma bora kwa ngazi zote,” Amesema Dkt.Maghembe
Aidha Naibu Katibu Mkuu,amebainisha kuwa Watoaji wa huduma wakibadilisha mitazamo yao katika syuala la ubora wa huduma wananchi watafurahia huduma wanazozipata kwakuzingatia maadili,utu heshima na huruma ili maboresho yaliyofanyika yaendane na utoaji wa huduma kwa wananchi ili waweze kufurahia huduma za afya.
Kwa upande wake Msajili wa Baraza la Madaktari Dkt. David Poul ameeleza suala la utoaji wa huduma kwa mteja katika taaluma ya afya ni muhimu ambalo lina hitaji kuzingatia misingi na heshima inayostahiki kwa wananchi.
Amesema mteja ndio sehemu ya huduma ya heshima ndani ya taaluma za afya wnaangalia waweke mikakati gani hasa kwakuendana na muiongozo na maadili yaliyopo ndani ya taaluma ili kutoa huduma bora.
“Kumuhudumia mteja nikumuangalia yeye na hali yake na kumfanya mteja aondoke eneo la huduma akiwa ameridhika”,Amesisitiza Dkt.David
Awali Msajili wa Baraza la Wauguzi,Agness Mtawa amesema kuwa watayafanyia akzi maagizo waliyopewa katika utoaji wa huduma bora kwa wateja katika utendaji kazi wao.