Waziri wa Habari ,Vijana, Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kuzindua mradi wa kukuza maendeleo ya kijamii (Alwaleed Philanthropies Project) kupitia elimu na mafunzo ya ufundi stadi yanayohusiana na utamaduni (TVET) na ajira chini ya ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO),huko Verde Mjini Unguja.
Waziri wa Habari ,Vijana, Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita akizungumza wakati akizindua mradi wa kukuza maendeleo ya kijamii (Alwaleed Philanthropies Project) kupitia elimu na mafunzo ya ufundi stadi yanayohusiana na utamaduni (TVET) na ajira chini ya ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO),huko Verde Mjini Unguja.
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO Michel Toto akitoa ufafanuzi juu ya mradi wa kukuza maendeleo ya kijamii (Alwaleed Philanthropies Project) kupitia elimu na mafunzo ya ufundi stadi yanayohusiana na utamaduni (TVET) na ajira wakati wa uzinduzi wa mradi huo huko Verde Mjini Unguja.
Na Fauzia Mussa, Maelezo
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amesema kuwepo kwa miradi ya kukuza maendeleo ya jamii kupitia ujasiriamali kutaongeza na kuzalisha ajira kwa Vijana.
Akizungumza wakati akizindua mradi wa kukuza maendeleo ya kijamii kupitia elimu na mafunzo ya ufundi stadi yanayohusiana na utamaduni (TVET) na ajira huko Verde Waziri Tabia amesema hatua hiyo itaongeza ubunifu wa kazi za sanaa na kurahisisha upatikanaji wa masoko ya kazi hizo
Amesema Vijana wengi wa Zanzibar wanajishuhulisha na kazi za sanaa na utamaduni ikiwemo uchongaji,uchoraji na muziki asilia hivyo Wizara itakua mstari wa mbele kuunga mkono juhudi za mradi huo ili kufikia malengo yaliokususdiwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt. Bakari Ali Silima amesema mradi huo umekuja wakati muafaka na utaongeza kasi ya utekelezaji wa mabadiliko ya elimu ambapo Wizara inakusudia kuifanya elimu ya amali kuwa ya lazima baada ya kukamilika kwa marekebisho ya sheria ya elimu ya mwaka 1982 na sera ya mwaka 2006.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Tanzania Nicolas Mkapa amesema mradi huo unaendana na matakwa halisi ya ajira kufuatia mageuzi ya mitaala ya elimu yanayotoa kipaombele katika stadi za kazi ili kukuza sanaa , ubunifu na tija .
Akitolea ufafanuzi juu ya mradi huo Amina majid kutoka Taasisi ya Al-Waleed na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO Michel Toto Wamesema Tanzania ni miongoni mwa wanufaika wa mradi huo unaofanya vizuri katika Nchi mbalimbali ikiwemo Nchi za Kiarabu na Agentina.
Mradi wa Al-waleed Philanthropies Project unaenda kutekelezwa na shirika la Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO .