Featured Michezo

LIVERPOOL HAISHIKIKI YAICHAPA BRIGHTON UGENINI

Written by mzalendoeditor

TIMU ya Liverpool wameendelea kuifukuzia Man City katika mbio za Ubingwa baada ya kung’ara ugenini kwa kupata ushindi wa mabao  2-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa The AMEX.
Mabao ya Liverpool yalifungwa na Luis Diaz dakika ya 19 na Mohamed Salah kwa penalti dakika ya 61 baada ya Yves Bissouma kuunawa mpira.
Kwa ushindi huo Liverpool inafikisha pointi 66, ingawa inabaki nafasi ya pili, ikizidiwa pointi tatu na Manchester City wanaoongoza, wakati Brighton inabaki na pointi zake 33 katika nafasi ya nane baada ya timu kucheza mechi 28.  

About the author

mzalendoeditor