Featured Kimataifa

SPIKA DKT.TULIA ATETA NA SPIKA WA BUNGE LA ANGOLA

Written by mzalendo

Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kwa Kundi la Afrika Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Angola Mhe. Carolina Cerqueira katika Ofisi za Spika huyo zilizopo Luanda nchini Angola leo tarehe 20 Oktoba, 2023

Pamoja na kumpongeza kwa mapokezi na maandalizi mazuri ya Mkutano wa 147 wa IPU unaotarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 23 Oktoba, 2023, Viongozi hao Wamekubaliana kuendeleza ushirikiano mzuri baina ya Mabunge hayo.

Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Mabunge Duniani kwa Kundi la Afrika (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akimkabidhi zawadi ya shukrani Spika wa Bunge la Angola Mhe. Carolina Cerqueira, wakati alipomtembelea ofisini kwake Jijini Luanda, Angola

Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Mabunge Duniani kwa Kundi la Afrika (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akifurahi jambo na Spika wa Bunge la Angola Mhe. Carolina Cerqueira, wakati alipomtembelea ofisini kwake Jijini Luanda, Angola

About the author

mzalendo