Featured Kitaifa

WATU WAWILI WAMEFARIKI DUNIA KWA AJALI MOROGORO

Written by mzalendoeditor

NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO

Watu wawili wamefikriki Dunia na wengine 43 kujeruhiwa kwenye ajali ya barabarani iliyohusisha Basi kampuni ya Abood yenye namba ya usajili T.326 DLS kugongana uso kwa uso na Lori la mzigo lenye namba za usajili T. 913 DKC lenye tela namba T.778 DKA aina ya Howo mali ya kampuni ya Dangote eneo la Maseyu Halmashauri ya Morogoro.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP.Alex Mkama amesema ajali hilo imetokea September 15 majira ya saa 5 eneo la Maseyu Kata ya Gwata Halmsahuri ya Morogoro ikihusisha basi kampuni ya Abood lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Morogoro kugongana uso kwa uso na lori mali ya Dangote lilikuwa likitoe Morogoro kwenda Dar res Salaam.

Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa Lori kutaka kupita magari mengine bila ya kuchukua tahadhari kisha kugongana na basi na kusababisha vifo vya watu wawili.

Abilai Issa Kamim Mganga Mfawidhi Hospitari ya Rufaa Mkoa wa Morogoro anasema wamepokea miili miwili ya marehemu ambayo ammoja ametamburika kwa majina ya Yusuphy Mzee ambaye ni Dereva wa lori na majeruhi 43, kati yao wawili wakipatiwa rufaa kwenda Hospitari ya Muhimbili kwa ajili ya matibatu zaidi.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanasema Basi la Abood lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Morogoro lilipofika eneo la Maseyu majira ya saa5 ndipo liligongana na lori hilo.

Hii ni ajali ya pili ndani ya mwezi wa tisa ilihusisha basi kampuni ya Abood kugangana na magari mengine ndanii ya mkoa wa Morogoro huku msisitizo uliopo ni madereva kuzingatia sheria za usalama barabrani ili kulinda masiha ya abilia na watumiaji wengine wa barabara.

About the author

mzalendoeditor