Featured Michezo

SIMBA SC YAZIDI KUGAWA DOZI LIGI KUU YA NBC

Written by mzalendoeditor
KLABU ya Simba SC imeendelea kugawa dozi katika Michezo ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kuichapa mabao 2-0 Dodoma Jiji FC mechi iliyopigwa   Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na washambuliaji wake Jean Othos Baleke dakika ya 43 na Mzambia, Moses Phiri dakika ya 55 huo ukiwa ushindi wa pili mfululizo ndani ya michezo miwili ya mwanzo baada ya kuichapa Mtibwa Sugar 4-2 Morogoro.

About the author

mzalendoeditor