Featured Michezo

YANGA SC YAANZA VYEMA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Written by mzalendoeditor

YANGA SC imeanza vyema Katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika Raundi ya Awali baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji ASAS ya Djibout mchezo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga SC yamefungwa na kiungo Mshambuliaji kutoka Burkina Faso, Stephane Aziz Ki dakika ya 22 na Mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia, Kennedy Musonda dakika ya 53.
Timu hizo zitarudiana Agosti 26 hapo hapo Chamazi Jijini Dar es Salaam na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla  kati ya Otoho ya Kongo Brazzaville na El Mereikh ya Sudan kuwania tiketi ya makundi.

About the author

mzalendoeditor