MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Poland, Robert Lewandowski ameweka rekodi ya kufunga hat-trick ya mapema kwenye historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana akiiwezesha Bayern Munich kutinga Robo Fainali kwa ushindi wa 7-1 dhidi ya RB Salzburg.
Katika mchezo huo wa marudiano Hatua ya 16 Bora usiku wa jana Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich, Lewandowski alitumia dakika ya 23 tu za mwanzo kufunga mabao yote matatu, akivunja rekodi iliyokwekwa Marco Simone ya kutumia dakika 24 kupiga hat-trick akiwa na AC Milan dhidi ya Rosenborg b mwaka 1996.
Lewandowski alifunga dakika ya 12 na 21 kwa penalti na lingine dakika ya 23, wakati mabao mengine ya Bayern Munich yalifungwa na Serge Gnabry dakika ya 31, Thomas Muller dakika ya 54 na 85 na Leroy Sané dakika ya 85, wakati bao pekee la RB Salzburg lilifungwa na Maurits Kjaergaard dakika ya 70.