Featured Kitaifa

WANAWAKE HAMASISHENI WANAUME KUPIMA UKIMWI

Written by mzalendoeditor

NA. Majid Abdulkarim, Mwanza

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maswala ya Ukimwi, Kifua Kikuu, Dawa za Kulevya na Magonjwa yasiyoya kuambukiza imetumia Siku ya Wanawake Duniani kuhamasisha wanaume nchini kujitokeza kupima ukimwi na kujua hali za afya zao kwa wakati ili watakao gundulika kupatiwa dawa.

Mhe. Toufiq amesema kuwa watakao gundulika watapatiwa dawa na wakatumia dawa hizo kwa ufasaha wataweza kufubaza virusi vya ukimwi na kufanya nchi kutokuwa na mbaambukizi mapya ya ugonjwa wa Ukimwi.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa kamati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maswala ya Ukimwi, Kifua Kikuu, Dawa za Kulevya na Magonjwa yasiyoya kuambukiza, Mhe. Fatma Toufiq wakati alipopata fursa ya kusalimia wanawake wa mkoa wa Mwanza katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Wilayani Nyamagana.

Akizungumza Mhe. Toufiq amesema kuwa inawezekana mwanaume akawa na maambukizi mke wake akawa hana maambukizi hivyo natoa shime kwa wanaume wote nchini kujitokeza kupima ukimwi ili kujua afya zenu, mkisha jua hali zenu maana yake ni kwamba mtapatiwa tiba sahihi.

“Takimwi zinaonyesha waathirika wengi wa maambukizi ya virusi vya ukimwi ni wanawake kwahiyo wanawake tuchukue tahadhari baadhi ya wanaume wengi hawaendi kupima ukimwi, wakipata matokeo kutoka kwa wake zao wanaamini kwamba wako salama”, ameeleza Mhe. Toufiq.

Mhe. Toufiq ameongeza kuwa Sasa ni shime kwa wanawake iwapo kama mwanamke utakuwa mwangalifu, mwaminifu na ukakataa ngono zembe inamaana kwamba swala zima la ukimwi litapungua na hakutakuwepo na maambukizi mapya nchini.

Pia Mhe. Toufiq amesisitiza kuwa kila mmoja alohudhuria maadhimisho hayo aweni balozi wa kuhakikisha kwamba Tanzania bila maambukizi ya ukimwi inawezekana, kila mtu mwenye umri wa kwenda kupima aende akapime , kuchukua tahadhari zote zile ambazo ni tabia hatarishi zinazoweza kusababisha kupatikana kwa maambukizi mapya.

“Wanawake wote serikali imejitahidi kwa uwezo wake wote kuhakikisha inatoa fursa mbali mbali ikiwemo mikopo ya wakina mama, kwahiyo kataeni kutumika , kataeni kutumiwa”, ameongeza Mhe. Toufiq.
Naye mwakilishi wa Mkuu wa mkoa Mwanza ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa mkoa huo Bw. Ngusa Samike amewataka wanawake kuhamasisha wanaume kupata tohara na kwa upande wa Watoto wadogo waweze kupatiwa tohara kwa wakati sahihi ili kudhibiti maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.

About the author

mzalendoeditor