Featured Kitaifa

RAIS SAMIA ATETA NA WAKE WA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU TUNGUU ZANZIBAR KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wake wa Viongozi mbalimbali katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Tunguu, Zanzibar tarehe 08 Machi, 2022 Siku ya kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na Mke wa Makamu wa Rais Mbonimpaye Mpango, Mke wa Rais wa Zanzibar Mariam Mwinyi pamoja na Wake wa viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya kuzungumza nao katika hafla fupi iliyofanyika katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 Machi, 2022 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Kitabu kutoka kwa Wake wa Viongozi mara baada ya kuzungumza nao katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Tunguu, Zanzibar katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 Machi, 2022 Sehemu ya Baadhi ya Wake za Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali waliohudhuria katika hafla fupi iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 Machi, 2022 iliyofanyika Ikulu Tunguu, Zanzibar. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi katika picha ya kumbukumbu pamoja na Waandaaji wa Filamu ya Kitanzania ya Binti.  Seko Shamte wa kwanza (Kushoto) ni Mtayarishaji/Producer wa filamu hiyo pamoja na Godliver Gordian muigizaji mkuu katika Filamu hiyo ambayo inaoneshwa na mtandaao maarufu wa Marekani wa kutazama filamu na vipindi vya runinga kupitia Mtandao (Netflix). 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya picha kutoka kwa mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango (kulia) pamoja na mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi katika hafla hiyo ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Ikulu Tunguu, Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango (kulia) pamoja na mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi mara baada ya hafla hiyo fupi ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Ikulu Tunguu, Zanzibar tarehe 08 Machi,2022.

 PICHA NA IKULU

About the author

mzalendoeditor