Featured Kitaifa

DKT. JINGU AKUTANA NA UNWOMEN KUJADILI MRADI WA WLE

Written by mzalendoeditor

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum Dkt. John Jingu amekutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la UN Women Hodan Addou kuhusu utekekezaji wa mradi wa uwezeshaji wanawake na wasichana kiuchumi na uongozi (WLER).

Mradi huo wa miaka minne (2022-2025) unaotekelezwa katika mikoa ya Arusha, Dar, es Salaam, Singida, Mtwara, Lindi na Pwani, unafadhiliwa na Serikali ya Ireland kwa ushirikiano na UN Women.

About the author

mzalendoeditor