Featured Kitaifa

WAZIRI MKUU:TUTAENDELEA KUIMARISHA AFYA YA MAMA NA MTOTO

Written by mzalendoeditor

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza, kwenye Mbio za Hisani za Benki ya NBC kuchangia ufadhili  kwa wanafunzi  wa masomo ya fani ya ukunga zilizofanyika jijini Dodoma.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya kuhakikisha kunakuwa na ustawi wa afya ya mama na mtoto ikiwemo mpango wa Mama Samia Mentorship Program.

Amesema kuwa mpango huo ni mahsusi kwa mafunzo ya muda mfupi kazini kwa madaktari bingwa na wakunga ili waweze kuimarisha utoaji huduma kwenye Vituo vya Afya na Hospitali za Wilaya.

Amesema hayo leo (Jumapili, Julai 23, 2023) aliposhiriki katika mbio za NBC ‘NBC Marathon’ zilizofanyika jijini Dodoma.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa mpango mwingine wa Serikali ni kuongeza wigo wa kutoa huduma za kupima dalili za awali za saratani ya uzazi kutoka Vituo vya Afya 925 vilivyopo hadi kufikia vituo vya Afya 1,025 hapa nchini.

“Mwingine ni kuimarisha wigo wa kutoa huduma za watoto wachanga kwa ujenzi wa wodi maalum, kununua vifaa tiba na mafunzo kwa watumishi kutoka hospitali 175 hadi kufikia hospitali 275 katika mwaka 2023/2024”.

Katika hatua nyingine Mheshimiwa Majaliwa ameitaka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo  kushirikiana  na sekta binafsi zenye lengo la kuinua michezo kama wanavyofanya NBC. 

“Suala hili lipewe kipaumbele kwani sote tunatambua kuwa michezo ni zaidi ya burudani na inachangia ajira na huduma za afya nchini”

Mbio za NBC kwa mwaka 2023 zinatarajia kukusanya Sh. milioni 300 ambazo zitatumika kuboresha afya ya mama na mtoto, kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake na kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa taaluma ya ukunga nchini ili kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa uzazi.

Naye, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo  Balozi Dkt. Pindi Chana amesema kuwa michezo ni nyenzo ya mabadiliko kwa jamii katika kuelimisha, kuimarisha afya na mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya

“Tutaendelea kushirikiana na wadau wa sekta binafsi na milango ya wizara ipo wazi. Lengo ni kupunguza wagonjwa wanaolazwa hospitali kwa kuhamasisha Watanzania kushiriki kwenye michezo ili kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza”

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishirki katika mazoezi ya viungo baada ya kuongoza Mbio za Hisani za Benki ya NBC kuchangia ufadhili  kwa wanafunzi  wa masomo ya fani ya ukunga zilizofanyika jijini Dodoma, Julai 23, 2023. Kushoto ni Waziri wa Utamaduni , Sanaa na Michezo, Balozi Dkt. Pindi Chana, kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi na wa tano kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishirki katika mazoezi ya viungo baada ya kuongoza Mbio za Hisani za Benki ya NBC kuchangia ufadhili  kwa wanafunzi  wa masomo ya fani ya ukunga zilizofanyika jijini Dodoma, Julai 23, 2023. Kushoto ni Waziri wa Utamaduni , Sanaa na Michezo, Balozi Dkt. Pindi Chana, kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza Mbio za Hisani za Benki ya NBC kuchangia ufadhili  kwa wanafunzi  wa masomo ya fani ya ukunga zilizofanyika jijini Dodoma, Julai 23, 2023. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamulwa, Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweli na kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza Mbio za Hisani za Benki ya NBC kuchangia ufadhili  kwa wanafunzi  wa masomo ya fani ya ukunga zilizofanyika jijini Dodoma, Julai 23, 2023. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweli na kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

– Advertisement –

Ad image

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akivishwa medali na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NBC, Dkt. Elirehema Doriye, kwenye Mbio za Hisani za Benki ya NBC kuchangia ufadhili  kwa wanafunzi  wa masomo ya fani ya ukunga zilizofanyika jijini Dodoma, Julai 23, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvika medali Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NBC, Dkt. Elirehema Doriye, kwenye Mbio za Hisani za Benki ya NBC kuchangia ufadhili  kwa wanafunzi  wa masomo ya fani ya ukunga zilizofanyika jijini Dodoma, Julai 23, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki mazoezi, kwenye Mbio za Hisani za Benki ya NBC kuchangia ufadhili  kwa wanafunzi  wa masomo ya fani ya ukunga zilizofanyika jijini Dodoma, Julai 23, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi hundi ya Shilingi Milioni Mia Moja, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dkt. Julius Mwaisalage, kwenye Mbio za Hisani za Benki ya NBC kuchangia ufadhili  kwa wanafunzi  wa masomo ya fani ya ukunga zilizofanyika jijini Dodoma, Julai 23, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi hundi ya Shilingi Milioni Tano, Mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita 21 (wanaume) Joseph Panga, kwenye Mbio za Hisani za Benki ya NBC kuchangia ufadhili  kwa wanafunzi  wa masomo ya fani ya ukunga zilizofanyika jijini Dodoma, Julai 23, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi hundi ya Shilingi Milioni Tano, Mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita 21 (wanawake), Magdalena Shauri, kwenye Mbio za Hisani za Benki ya NBC kuchangia ufadhili  kwa wanafunzi  wa masomo ya fani ya ukunga zilizofanyika jijini Dodoma, Julai 23, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, kwenye Mbio za Hisani za Benki ya NBC kuchangia ufadhili  kwa wanafunzi  wa masomo ya fani ya ukunga zilizofanyika jijini Dodoma, Julai 23, 2023. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NBC, Dkt. Elirehema Doriye. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

About the author

mzalendoeditor