Featured Michezo

MWENYEKITI GEREFA AIPONGEZA TIMU YA VIJANA YA GEITA GOLD KWA KUFIKIA HATUA YA LIGI YA VIJANA TFF.

Written by mzalendoeditor

Na Joel Maduka Geita…
Mwenyekiti wa chama cha Mpira wa miguu Mkoa wa Geita (GEREFA) Ndg  Salum Kulunge ameipongeza timu ya vijana ya   Geita Gold U20 iliyofanikiwa kuingia fainali ya mashindano ya ligi kuu kwa timu za vijana chini ya umri wa miaka 20.
 
Timu ya vijana ya Geita Gold  imeingia kwenye  hatua ya fainali ya Ligi ya vijana ya Tff inayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es Salaam,ambapo leo jumapili  tar 2 July  inatarajia kucheza na timu ya Kagera Sugar kwenye uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi.
 
 Kupitia mchezo huu wa leo Mwenyekiti  Kulunge ametumia nafasi hiyo kuwatakia kila la kheri kikosi cha vijana cha Geita Gold ambacho kinacheza na Mtigwa Suger majira ya saa 12 jioni.
Amesema wanauhakika  timu hiyo itafanya vizuri kutokana na  ubora wa timu na benchi la ufundi chini ya kocha Mkuu Mwl Choke Abeid na kwamba inaenda   kuandika historia nyingine kwenye tasnia ya michezo hapa nchi kwa kulitwa kombe .
 
“Binafsi na kwa niaba ya chama niseme Tumefarijika sana na mafanikio makubwa ya maendeleo ya soka la vijana wetu wa  mkoani Geita,Tukumbuke kuna timu yetu ya Umiseta Mkoa imefanikiwa kutwaa ubingwa wa UMISETA Taifa na kwenye soka la wasichana tumekua washindi wa tatu Taifa leo hii timu yetu ya  vijana inacheza fainali kwa timu za ligi kuu Vijana kwetu sisi tunaona ni hatua kubwa kwenye soka”Salum Kulunge Mwenyekiti wa GEREFA.
 
Kulunge ameongezea  mikakati  ya Gerefa ni kuona vijana wanapatiwa usajiri kwenye timu kubwa ya Geita Gold.
 
“Lengo letu kubwa la kushirikiana na  kuzipandisha timu hizi mbili kubwa ligi kuu ni lengo la kusaidia vipaji vya vijana wetu  Unajua Geita tuna bahati kubwa ya kua na vijana wenye vipaji vya hali ya juu ktk tasnia ya soko ndio maana tumejiwekea mikakati ya hali ya juu kusaidia kuwaendeleza”Salum Kulunge Mwenyekiti wa GEREFA .
 
Sanjali na hayo Kulunge amewaomba wadau wengine wapenda soka kuendelea kuzifadhiri timu ambazo zimeendelea kufanya vizuri ndani ya Mkoa wa Geita kwa kutoa vitu mbali mbali ambavyo vitawasaidia kwenye mahitaji ya msingi.

About the author

mzalendoeditor