Featured Kitaifa

ASILIMIA 30 YA WATOTO WANAKABILIWA NA UDUMAVU WA AKILI KUTOKANA NA LISHE DUNI

Written by mzalendoeditor

 

Naibu katibu mkuu kutoka Ofisi ya Rais-Tamisemi,Wilson Mahela,akizungumza wakati akifunga  Mafunzo ya Sayansi ya Malezi na Makuzi kwa maafisa Ustawi na Maendeleo ya Jamii yaliyofanyika kwa siku tano,Mkoani Dodoma kuanzia Juni 26-Julai 1 2023.

Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu katibu mkuu kutoka Ofisi ya Rais-Tamisemi,Wilson Mahela (hayupo pichani) ,akizungumza wakati akifunga  Mafunzo ya Sayansi ya Malezi na Makuzi kwa maafisa Ustawi na Maendeleo ya Jamii yaliyofanyika kwa siku tano,Mkoani Dodoma kuanzia Juni 26-Julai 1 2023.

Mwakilishi wa Shirika la Crossfire ,Frank Samson akingumza wakati wa kufunga Mafunzo ya Sayansi ya Malezi na Makuzi kwa maafisa Ustawi na Maendeleo ya Jamii yaliyofanyika kwa siku tano,Mkoani Dodoma kuanzia Juni 26-Julai 1 2023.

Mkurugenzi wa idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka wizara ya Maendelo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi maalum,Sebastian Kitiku akizungumza katika hitimisho la mafunzo ya sayansi ya Malezi na Makuzi kwa maafisa Ustawi na Maendeleo ya Jamii yaliyofanyika kwa siku tano,Mkoani Dodoma kuanzia Juni 26-Julai 1 2023.

Mkurugenzi wa Mtandao wa Malezi na Makuzi (TECDEN) akizungumza wakati wa kufunga la Mafunzo ya Sayansi ya Malezi na Makuzi kwa maafisa Ustawi na Maendeleo ya Jamii yaliyofanyika kwa siku tano,Mkoani Dodoma kuanzia Juni 26-Julai 1 2023.

Naibu katibu mkuu kutoka Ofisi ya Rais-Tamisemi,Wilson Mahela,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufunga   Mafunzo ya Sayansi ya Malezi na Makuzi kwa maafisa Ustawi na Maendeleo ya Jamii yaliyofanyika kwa siku tano,Mkoani Dodoma kuanzia Juni 26-Julai 1 2023.

NA.Dotto Kwilasa-DODOMA

Licha ya juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali kuhamasisha jamii ulaji wa chakula bora,bado asilimia 30 ya watoto wenye umri kuanzia siku 0 hadi miaka 8 wanakabiliwa na udumavu wa akili kutokana na kukosa lishe.

Aidha Mikoa yenye uzalishaji mkubwa wa chakula inatajwa kuongoza kuwa na watoto wengi wenye udumavu wa akili.

Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt.Wilson Mahera amesema hayo  July 1,2023 wakati wa kufunga mafunzo ya Kitaifa ya sayansi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto yaliyofanyika jijini Dodoma kwa muda wa siku sita.

Dk. Mahela amesema kutokana na takwimu hizo serikali imeona kuwepo kwa umuhimu wa kupambana na hali hiyo ili kuweza kupata watoto ambao wakatuwa na utimilifu wa akili jambo ambalo alisema kuwa litasidia kuwa na taifa lenye watu wanaoweza kuzalisha na kulitafa taifa kuwa na viongozi bora.

Amesema licha ya kuhakikisha watoto wa umri huo wanapatiwa lishe bora pia watoto wanatakiwa kulindwa na kupewa uhuru wa kuweza kujieleza na kueleza na siyo kuwafanya kuwa watu wa kuelezwa tu.

“Wapo wazazi ambao wanadhani malezi ni kuwapiga watoto tu na kuwafanya kuwa wa kuelezwa badala ya kujieleza, wazazi walezi mnatakiwa kutambua kuwa mtoto anatakia kupewa nafasi ya kujieleza na kueleza na kuondokana na tabia ya kuwapiga watoto viboko badala ya kuwapa uwanja mpana wa kujieleza.

“Watoto msiwafanye kuwa na nithamu ya uwoga badala yake wapeni uhuru wa kujieleza lakini wazoesheni kula vyakula ambavyo vinawajenga kiakili ikiwemo samaki,nyama,nyama ya kuku au nyama yoyote chakula kiwe nyama alafu vyakula vingine viwe za ziada” ameeleza Dk.Mahera.

Amesema Serikali inataka Jamii kuwalea watoto wao katika malezi na Makuzi hususani kuwapa lishe Bora ili kuwatengenezea mazingira mazuri Kwenye maisha yao ya badae ambapo mtoto asipolelewa vizuri husababisha udumavu kimwili, kiakili na kisaikolojia.

Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya Kitaifa ya sayansi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto akiwemo Afisa ustawi wa jamii Mkoa wa Manyara Khadija Muwango na Musa Masongo wa shirika la TAHEA Mwanza wamesema mafunzo hayo ni muhimu kwao kwa na kwamba wataenda kutoa elimu hiyo kwa jamii.

“Tunahitaji kuona mtoto anakua vizuri kimwili na kiakili,mtoto anahitaji chakula bora na mlo kamili,hivyo vyote vinajumuisha vyakula vyenye virutubisho kama protini, wanga, mafuta, vitamini na madini,”wameeleza washiriki hao.

About the author

mzalendoeditor