Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kamba pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuashiria ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino huku viongozi mbalimbali wakishuhudia katika Sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Na.Alex Sonna-CHAMWINO
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua jengo jipya la Ikulu ya Chamwino na kusisitiza serikali imehamia Dodoma na Dar es salaam itabaki kuwa Jiji la kibiashara.
Rais Samia ameyasema hayo Leo Mei 20,2023 Ikulu Chamwino Dodoma kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo hilo ambalo ni ofisi za Rais zilizojengwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na yamesanifiwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA) ambaye pia ni mshauri elekezi.
“Hii ni Ikulu ya watanzania na tunajivunia kwa sababu ni nguvu ya watanzania kwani imejengwa na watanzania wenyewe mchakato wa kuhamia Dodoma ulianza mapema na umepitia katika ngazi mbalimbali tangu mwaka 1966 ambapo Joseph Nyerere mdogo wake na Rais wa awamu ya kwanza Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere alipopeleka hoja bungeni ya kutaka Dodoma kuwa makao makuu na hoja yake ilipingwa.
Awamu zote zilianza kujenga Ofisi mbalimbali za Serikali na Taasisi zake ambapo katika awamu ya tano ndipo msukumo ulipoongezeka.
Dkt.Samia ameahidi kuwa atahakikisha Miradi yote iliyokuwa imeanza kutekelezwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Hayati Dkt.John Pombe Magufuli itakamilika huku akisema huo ni mradi wa pili kukamilika baada ya Daraja la Tanzanite.
“Kukamilika kwa ujenzi wa Ikulu hii ni ishara kuwa sasa Serikali imehamia Dodoma kwa maana hiyo Dar es Salaam itakuwa tunakwenda tu kupokea wageni wetu wa Kimataifa na tukikamilisha Ujenzi wa uwanja wa ndege wa kiimataifa wa Msalato wageni wote tutakuwa tunawapokea hapa hapa na Dar es salaam tutaiacha kama mji wa kibiashara,”amesema Dkt.Samia
Naye Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango amewataka watumishi wa Ikulu kuheshimu na kutunza vizuri jengo la Ofisi ya Ikulu lililozinduliwa ili litumike kutoa maamuzi ya kuamua hatma ya Tanzania na kuwezesha kusonga mbele.
Naye Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka amesema Ikulu hiyo mpya imejengwa na wazawa ikiwa ni baada ya miaka 100 tangu Ikulu ya Dar es Salaam iliyojengwa na wakoloni mwaka 1923.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba yake mara baada ya kufungua rasmi Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na Marais Wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Ali Hassan Mwinyi, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Pamoja na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuzindua Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdalla pamoja na Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi wakati akikata Utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdalla pamoja na Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi wakati akikata Utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango wakati wakipiga ngoma kabla ya kuingia Rasmi katika Ofisi za Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Rasmi la Ukaguzi lililoandaliwa na Jeshi la Polisi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Viongozi wa Serikali, Viongozi wastaafu, watu mashuhuri pamoja na wananchi wengine wakiwa katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma kwa ajili ya Sherehe za ufunguzi wa Jengo la Ikulu Chamwino tarehe 20 Mei, 2023.
Taaswira ya Jengo jipya la Ikulu ya Chamwino kama linavyoonekana pichani ambalo limezinduliwa Rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Tuzo ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa Mama Maria Nyerere wakati wa Sherehe za ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Tuzo ya Hayati Rais wa Awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa Mama Janeth Magufuli wakati wa Sherehe za ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba yake mara baada ya kufungua rasmi Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson pamoja na Spika wa Baraza la Waakilishi Mhe. Zubeir Ally Maulid mara baada ya kufungua Jengo la Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango pamoja na viongozi wengine wakati wakiangalia juu wakati Bendera ya Taifa, ya Rais na ile ya Afrika Mashariki ikipandishwa mara baada ya ufunguzi wa Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Mei, 2023.