Featured Kitaifa

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA USTAWI NA MAENDELEO YA JAMII YAISHAURI SERIKALI

Written by mzalendoeditor

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Bi Fatma Tawfiq akizungumza wakati wa Kikao kazi kilichofanyika kati ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Bunge ya Huduma ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii na Wakurugenzi  kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum jijini Dodoma tarehe 11/03/2023.

Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum Dkt John Jingu akizungumza wakati wa kikao kazi kilichofanyika kati Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Bunge ya Huduma ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii na Wakurugenzi  kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum jijini Dodoma tarehe 11/03/2023.

Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Bunge ya Huduma ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe. Ali Hassan Omar Kingi akizungumza wakati wa Kikao Kazi kati ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Bunge ya Huduma ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii na Wakurugenzi  toka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake  na Makundi Maalum jijini Dodoma tarehe 11/03/2023.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Bunge ya Huduma ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii walipokutana na Viongozi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum jijini Dodoma tarehe 11/03/2023.

 

Baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Katika Mkutano na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Bunge ya Huduma ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii jijini Dodoma tarehe 11/03/2023. 
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM
Na WMJJWM, Dodoma
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe. Fatma Tawfiq ameishauri Serikali kutenga bajeti ya kutosha katika kutekeleza majukumu ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
Mhe. Tawfiq ametoa ushauri huo wakati wa Kikao kazi cha Kamati hiyo na Wizara kilichofanyika Machi 11, 2023 jijini Dodoma.
Mhe. Tawfiq amesema Kamati za utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) zilizopo ngazi ya vijiji na Mitaa hazifanyi kazi ipasavyo moja ya sababu ni kukosa bajeti hivyo kuchangia vitendo vya ukatili kunaongezeka.
“Kamati za MTAKUWWA ngazi ya Jamii mziangalie kwani zenyewe ndio chanzo cha kutoa taarifa kuhusiana na masuala ya ukatili kwa sababu yanaanzia katika ngazi ya familia ambako ndugu  wanalindana. Hili jambo tuangalie Kamati hizi zipate nguvu ya kutosha” amesema Mhe. Tawfiq.
Ameongeza kuwa Wizara bado ina kazi kubwa hasa katika upande wa mila na desturi potofu zinazochangia ukatili wa kijinsia na watoto.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu ameieleza Kamati hiyo kwamba Wizara imeendelea kuimarisha mifumo ya ulinzi wa Wanawake na Watoto katika kukabiliana na ukatili wa kijinsia na watoto na kujenga uelewa wa Jamii.
“Jamii imeelewa na kuhamasika kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia na watoto ambapo Jamii imeunga mkono Kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii katika mikoa yote 26 Tanzania bara ambayo inaratibiwa na Wizara pamoja wadau mbalimbali, hadi sasa wananchi 8319 wamejiunga na kampeni hii inayojilulikana kwa ufupi SMAUJATA” amesema Dkt. Jingu.
Dkt. Jingu pia amebainisha baadhi ya changamoto zinazoikabili Wizara ni pamoja na uhaba wa Maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa, mila na Desturi potofu pamoja na Mila za kigeni zinazochangia kumomonyoka kwa maadili na udhaifi wa utoaji wa baadhi ya huduma kwa wahanga wa ukatili.
“Kuna uhaba wa Maafisa Ustawi wa Jamii 21,204 na Maafisa Maendeleo ya Jamii 2,320, ukosefu wa taarifa sahihi za wafanyabiashara ndogo ndogo zinazochangia kushindwa kuwatambua na kuwaunganisha na fursa za Maendeleo, kuendelea kuwepo kwa Mila na Desturi zenye madhara katika baadhi ya Jamii” amesema Dkt. Jingu.
Naye mjunbe wa Kamati ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe. Sophia Mwakagenda amesema Wizara ina dhamana kubwa ya kuhudumia jamii hivyo ni muhimu kutengewa bajeti itakayowezesha kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
“Kwa uzoefu changamoto kubwa ni bajeti, kwa hiyo kama Kamati tunayo kazi kubwa ya kuhakikisha bajeti ya Wizara hii tunaipambania kwa maslahi ya Taifa kwa sababu inahusiana na maisha ya watu” mmesema Mhe. Sophia.
Kamati hiyo mpya ambayo imeundwa hivi karibuni, imeahidi kutoa ushirikiano kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

About the author

mzalendoeditor