Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo amewasili Singida Vijijini (Wilaya ya Kichama) tayari kwa ziara ya kuimarisha Chama pamoja na kukagua, kuhimiza na kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema pamoja na Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi (Gavu).