Featured Michezo

WAZIRI CHANA ASHUHUDIA FOUNTAIN GATE IKITWAA UBINGWA WA CECAFA CHINI YA MIAKA 15

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Februari 19, 2023 ameshuhudia timu ya Fountain Gate ikitwaa Ubingwa wa CECAFA umri chini ya miaka 15, baada ya kuifunga timu ya Awaro kutoka Ethiopia, mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Azam complex.

Fountain Gate wameibuka Bingwa baada ya kuichapa Awaro magoli 3 – 0.

Mechi hiyo imeshuhudiwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Saidi Yakubu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Wallace Karia na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Ally Mayay.

About the author

mzalendoeditor