Featured Kitaifa

TAMASHA LA USIKU WA HABARI DODOMA LAWEKA HISTORIA TUZO MBALIMBALI ZATOLEWA

Written by mzalendoeditor

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew,akimkabidhi Tuzo ya Mwandishi Bora wa Mwaka Mkoa wa Dodoma Augusta Njoji kutoka Gazeti la Nipashe kwa taarifa aliyotoa imeonyesha Jitihada binafsi iliyotolewa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma wakati wa  tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) .

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew,akizungumza wakati akifungua tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule,Viongozi wa Vyama vya Siasa, waandishi wa Habari wa mkoa huo na wadau mbalimbali wa sekta hiyo lililofanyika jijini Dodoma.
SEHEMU ya Waandishi wa habari pamoja na Wadau wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew,wakati akifungua tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule,Viongozi wa Vyama vya Siasa, waandishi wa Habari wa mkoa huo na wadau mbalimbali wa sekta hiyo lililofanyika jijini Dodoma.

MKUU  wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule,akizungumza wakati wa tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) lililofanyika jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma Bw.Mussa Yusuph,akizungumza wakati wa tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) lililofanyika jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa Kamati  ya Maandalizi Bi.Sakina Abdulmasoud,akielezea lengo la tamasha hilo wakati wa tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) lililofanyika jijini Dodoma.

MKURUGENZI Mtendaji wa WazoHuru Media Bw.Mathias Canal,akizungumza wakati wa tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) lililofanyika jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa Kamati ya Tuzo Bi.Nelly Mtema,akizungumzia mchakato wa kuwapata washindi wa tuzo wakati wa tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) lililofanyika jijini Dodoma.

KATIBU wa Klabu ya Waaandishi wa habari Mkoa wa Dodoma Ben Bago,akizungumza wakati wa tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) lililofanyika jijini Dodoma.

KATIBU  wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga,akizungumza wakati wa tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) lililofanyika jijini Dodoma.

MBUNGE  wa Viti maalum Mkoa wa Dodoma Fatma Toufiq,akizungumza wakati wa tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) lililofanyika jijini Dodoma.

AFISA Habari Kanda ya Kati wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bw.Juma Omary ,akizungumza wakati wa tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) lililofanyika jijini Dodoma.

WAANDISHI wa Habari Mkoa wa Dodoma wakionyesha ubunifu wa Mavazi wakipita mbele ya Mgeni rasmi Naibu  Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew wakati wa  tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule,Viongozi wa Vyama vya Siasa, waandishi wa Habari wa mkoa huo na wadau mbalimbali wa sekta hiyo lililofanyika jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew,akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mhe.Rosemary Senyamule,Viongozi wa Vyama vya Siasa, waandishi wa Habari wa mkoa huo na wadau mbalimbali wa sekta hiyo wakisakata rumba wakati wa tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC)  lililofanyika jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew,akizindua Kikoba cha waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma wakati wa tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule,Viongozi wa Vyama vya Siasa, waandishi wa Habari wa mkoa huo na wadau mbalimbali wa sekta hiyo lililofanyika jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew,akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kufumgua Kikoba cha waandishi hao wakati wa tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule,Viongozi wa Vyama vya Siasa, waandishi wa Habari wa mkoa huo na wadau mbalimbali wa sekta hiyo lililofanyika jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew,akimkabidhi Tuzo ya Heshima  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule iliyotolewa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutambua mchango wake katikka Tasnia ya Habari wakati wa  tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) .

MWENYEKITI wa Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma Bw.Mussa Yusuph akimkabidhi tuzo Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew,kwa kutambua mchango wa Wizara katika Tasnia ya Habari wakati wa  tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule,Viongozi wa Vyama vya Siasa, waandishi wa Habari wa mkoa huo na wadau mbalimbali wa sekta hiyo lililofanyika jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew,akimkabidhi Tuzo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule iliyotolewa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma kwa kutambua ushirikiano wanaowapa katika kutekeleza majukumu yao wakati wa  tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) .

 

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew,akikabidhi Tuzo mbalimbali kwa Wadhamini wa tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule,Viongozi wa Vyama vya Siasa, waandishi wa Habari wa mkoa huo na wadau mbalimbali wa sekta hiyo lililofanyika jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew,akimkabidhi Tuzo ya Afisa bora wa mwaka Mkoa wa Dodoma Nteghenjwa Hosea kutoka Ofisi ya TAMISEMA iliyotolewa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma wakati wa  tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule,Viongozi wa Vyama vya Siasa, waandishi wa Habari wa mkoa huo na wadau mbalimbali wa sekta hiyo lililofanyika jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew,akimkabidhi Tuzo ya Mwandishi Bora wa Mwaka Mkoa wa Dodoma Augusta Njoji kutoka Gazeti la Nipashe kwa taarifa aliyotoa imeonyesha Jitihada binafsi iliyotolewa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma wakati wa  tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) .

 Mwandishi Bora wa Mwaka Mkoa wa Dodoma Augusta Njoji kutoka Gazeti la Nipashe akiwa na tuzo yake pamoja na marafiki zake wakiangalia tuzo hiyo  iliyotolewa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma kwa taarifa aliyotoa imeonyesha Jitihada binafsi wakati wa  tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) .

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew,akimkabidhi Tuzo ya Mwanachama bora wa klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma kwa kulipa na Kuonyesa ushirikiano mzuri na wenzake   iliyotolewa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma wakati wa  tamasha la usiku wa Habari Dodoma.

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew,akimkabidhi Tuzo Mwandishi Chipukizi Rasul Kidindi ambaye amekuwa tayari kujifunza,ana nidhamu,yupo makini na ana ushirikiano na wenzake   iliyotolewa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma wakati wa  tamasha la usiku wa Habari Dodoma.

MWANDISHI Mwandamizi Mkoa wa Dodoma Alhaj Idd Maalimu,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya waandishi kwa Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew (hayupo pichani) mara baada ya kufungua  tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule,Viongozi wa Vyama vya Siasa, waandishi wa Habari wa mkoa huo na wadau mbalimbali wa sekta hiyo lililofanyika jijini Dodoma.     

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew,akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma mara baada ya kufungua  tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule,Viongozi wa Vyama vya Siasa, waandishi wa Habari wa mkoa huo na wadau mbalimbali wa sekta hiyo lililofanyika jijini Dodoma.

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew,akiwa katika picha ya pamoja na Wadhamini,Wadau na Viongozi wa Siasa Mkoa wa Dodoma mara baada ya kufungua  tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule,Viongozi wa Vyama vya Siasa, waandishi wa Habari wa mkoa huo na wadau mbalimbali wa sekta hiyo lililofanyika jijini Dodoma.

PICHA ZOTE NA ALEX SONNA

Na Innocent Natai, WazoHuru Media-Dodoma
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha mazingira mazuri ya tasnia ya Habari nchini.
Amebainisha kuwa katika kipindi kifupi tangu aingie madarakani tasnia ya habari imeimarika, waandishi wa Habari wamekuwa na uhuru wa kutoa Habari na kupata Habari kwa urahisi.
Akizungumza tatehe 17 Februari, 2023 wakati akifungua tamasha la usiku wa Habari Dodoma lililoandaliwa na Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (CPC) na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Rosemary Senyamule,Viongozi wa Vyama vya Siasa, waandishi wa Habari wa mkoa huo na wadau mbalimbali wa sekta hiyo, Mhandisi Kundo amesema kuwa kipaumbele kikubwa cha mwanahabari ni kupata habari hivyo kukosa fursa hiyo hatoweza kufanya kazi yake.
Amesema kuwa Mhe Rais ameonyesha nia ya dhati ya kuisaidia tasnia ya habari kwa kufanya mambo makubwa ikiwemo kuandaa mchakato wa kuendelea kuangalia marekebisho ya sheria ya habari ambapo anaamini pindi utakapokamilika wanahabari watakwenda kufanya kazi zao kwa uhuru bila kuwa na changamoto yeyote.
“Haya mazingira mazuri ya tasnia ya Habari Mheshimiwa  Rais ameyaweka vizuri katika misingi ya kisheria ili muweze kuhakikisha mnahabarisha Watanzania kuhusu utekelezaji wa mambo yote yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita” almmesema Mhe. Mhandisi Kundo
Ameongeza kuwa wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeweka mikakati ya kutazama uchumi wa wanahabari na vyombo vya habari ili kuona kwa namna gani taifa linaweza kutembea kwa pamoja kiuchumi. 
Aidha amewapongeza waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma kwa kutangaza vyema Mkoa wa Dodoma na shughuli za bunge hivyo kuwafikishia vyema taarifa wananchi na wapiga kura majimboni kwao.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amesema kuwa Mheshimiwa Rais amewakumbusha viongozi wa serikali kuwa Haki ya kutoa habari kwa wanahabari ni haki ya msingi na ameelekeza kutolewa kwa habari zinazohitajika na Waandishi kwa manufaa ya nchi.
Aidha ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Waandishi wa Habari kwa kuwapa habari ili kuwarahisishia mazingira ya kazi kwani mkoa wa Dodoma unatambua mchango mkubwa kutoka kwa waandishi kwani wamekuwa chachu ya kutangaza shughuli zinazofanywa kila siku na serikali kupitia Mkoa huo.
Akitoa Shukrani kwa niaba ya Waandishi Ndugu Mathias Canal ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa WazoHuru Media amesema kuwa ni jambo zuri na upekee alilolifanya Mheshimiwa Rais kwa wanatasnia wa habari kwani sasa kuanzisha kwa vyombo vya habari nchini imekuwa si jambo la kawaida tena bali imekuwa ni fursa nyingine ya vijana kujiajiri.
Aidha amewapongeza waandishi wa Habari hao kwa kuanzisha kikundi cha kujikwamua kiuchumi kwa kuwekeza fedha kupitia KIKOBA ambacho punde kitakapoimarika wataanzisha Chama cha Akiba na mikopo (SACCOS)

About the author

mzalendoeditor