Featured Kitaifa

RC SENYAMULE AFUNGUA MAFUNZO YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA MKOA WA DODOMA 

Written by mzalendoeditor

 

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Baadhi ya Viongozi Wapya Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika leo Februari 8,2023 jijini Dodoma.

KATIBU  Ukuzaji Maadili Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bw.Waziri Kipacha,akitoa taarifa ya mafunzo hayo wakati wa Mafunzo ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Baadhi ya Viongozi Wapya Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika leo Februari 8,2023 jijini Dodoma.

KATIBU  Msaidizi -Kanda ya Kati,Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bi.Jasmin Awadhi Bakari,akizungumza wakati wa Mafunzo ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Baadhi ya Viongozi Wapya Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika leo Februari 8,2023 jijini Dodoma.

SEHEMU ya Viongozi Wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,(hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Baadhi ya Viongozi Wapya Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika leo Februari 8,2023 jijini Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mafunzo ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa Baadhi ya Viongozi Wapya Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika leo Februari 8,2023 jijini Dodoma.

……………………………….

 

Na Alex Sonna-DODOMA

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewataka Viongozi wapya wateule wa Rais kuhakikisha kuwa wanawajibika kwa ukamilifu ili kuweza kufikia malengo ya dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.

Hayo ameyasema leo Februari 8,2023 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa baadhi ya viongozi wapya wa serikali ambapo amesema  kuwa ni vizuri watumishi wakakuza utamaduni wa uadilifu na uwajibikaji.

Senyamule amesema kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 inalenga pamoja na mambo mengine kuwa taifa lenye maadili linaloheshimu utawala wa sheria na lisilokuwa na Rushwa.

“Tunapozungumzia suala la Maadili kwa Viongozi wa Umma sio tuu kutoa matamko ya rasilimali na madeni, kuna kuwajibika, uadilifu, uwazi, kuheshimu sheria, kujali watu wengine, kuzuia tamaa, kuepuka upendeleo na mgongano wa maslahi” amesema Senyamule.

Aidha  Senyamule ameipongeza ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kuandaa mafunzo haya na kusema kuwa jitihada za kufanikisha mafunzo haya ni kielelezo cha dhamira ya dhati ya serikali ya Awamu ya Sita kuhakikisha kuwa suala la maadili kwa viongozi wa Umma linaeleweka vizuri ili kukuza utawala bora nchini.

“Maadili ni nyenzo muhimu sana katika kuliimarisha Taifa na kuliepusha kuingia katika mifarakano na migogoro isiyo ya lazima kwani hujenga umoja, Amani, upendo, uvumilivu, mshikamano na utii wa sheria bila shuruti mambo yanayochangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Taifa” amesema

Ameitaka pia Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuendelea kuhakikisha kuwa viongozi wa Umma wanazingatia misingi yote ya maadili na pale watakapokiuka basi wachukuliwe hatua kulingana na sheria za maadili ya utumishi wa umma.

Kwa upande wake Katibu wa Ukuzaji Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma Bw. Waziri Kipacha amesema kuwa mafunzo haya yanalenga kuwaelimisha viongozi wapya katika utumishi wa umma juu ya sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Uwajibikaji wa pamoja katika sekta ya Umma pamoja na kanuni za udhibiti wa Mgongano wa maslahi.

Ameongeza kuwa viongozi wapya wataelimishwa pia kanuni za ahadi ya uadilifu na utoaji tamko la rasilimali na madeni.

“Tunatarajia mafunzo haya yatawaongezea viongozi wetu uelewa kuhusu misingiya uwajibikaji, maadili pamoja na kuepuka mgongano wa maslahi lakini pia tutafanya tathmini ili kuona uelewa wa viongozi wetu kabla na baada ya mafunzo” amesema Kipacha.

About the author

mzalendoeditor