Featured Kitaifa

DIT NA TAASISI YA CQVIE KUTOKA CHINA ZASAINI MAKUBALIANO KATIKA ELIMU

Written by mzalendoeditor

 

Na WyEST,DSM

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameshuhudia utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na Taasisi ya Ufundi ya Chonqing (CQVIE) kutoka nchini China.

Waziri Mkenda amesema ushirikiano huo umekuja wakati muafaka Tanzania ikiwa katika mchakato wa MAGEUZI makubwa katika elimu.

Miongoni mwa makubaliano ya ushirikiano baina ya Taasisi hizo ni kubadilishana Wanafunzi na Walimu (exchange program ) ili kubadilishana uzoefu katika ujuzi wanaopata katika mafunzo.

Pia wanafunzi wanufaika wa programu hiyo watakuwa na sifa za kufanya kazi katika makampuni mbalimbali nchini China.

Prof. Mkenda amesema Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itahakikisha ushirikiano huo unadumu na unakuwa endelevu kwa maslahi ya nchi hizo mbili.

About the author

mzalendoeditor