Featured Kitaifa

DC ARUSHA WAZAZI MSIWAFICHE WATOTO KUTOPATA CHANJO YA POLIO NI KWA USALAMA WA MTOTO

Written by mzalendoeditor
Mkuu wa wilaya ya Arusha Said Mtanda akimpa chanjo ya pilio mmoja wa watoto waliofika katika kituo Cha afya daraja mbili.
……………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Said Mtanda amewataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kupata chanjo ya Polio katika vituo vya afya na sio kuwaficha ndani kwani chanjo hiyo ni kwaajili ya  kuhakikisha usalama wa makuzi bora kwa mtoto.
Mtanda ameyasema hayo katika uzinduzi wa chanjo ya polio katika kituo cha afya daraja mbili kilichopo jijini Arusha ambapo amebainisha kuwa chanjo hiyo ni salama haina madhara yoyote na inatolewa bure kwa lengo la mkuzi bora ya mtoto.
“Matarajio yetu ni kuwachanja watoto wote waliochini ya miaka mitano ili kuhakikisha usalama na afya ya mtoto inahimarika na asitokee mzazi au mlezi anamzuia mtoto kupatiwa chanjo hii itakuwa ni kinyume na serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania juu ya afya njema ya mtoto,”alisema Mtanda.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha Hergney Chitukulo alisema katika awamu ya kwanza takribani watoto 93000 walichanjwa ikiwa awamu ya pili ni 111808 na mwitikio huu inamaanisha elimu imeeleweka na wananchi wameelewa umuhimu wa chanjo hiyo.
“Wazazi wametuelewa kwa kufahamu umuhimu wa kuchanja watoto kwa ajili ya maisha ya watoto na hii inawasaidia wazazi kuwapunguzia adha ya matibabu mara kwa mara kutokana na mtoto kuwa na kinga ya polio,”alisema.
Hata hivyo alisisitiza wazazi kutumia kikamilifu siku nne hizo zilizotolewa na serikali kuwapeleka katika vituo vya afya ili waweze kupata chanjo ya polio .
Nao baadhi ya wazazi na walezi wa wilaya ya Arusha walisema chanjo hiyo ni muhimu kwa watoto wao kwani itawasaidia katika kuwakinga watoto wao wasipate ugonjwa huo wa polio.
Kauli mbiu  ni kila tone la chanjo ya polio litaiweka Tanzania salama dhidi ya ugonjwa wa kupooza, Mpe matone okoa maisha.

About the author

mzalendoeditor