MWENYEKITI wa Tume ya Watumishi wa Umma ,Jaji Mstaafu Hamisa Kalombola, akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya chamwino Mkoani Dodoma wakati wa ziara ya Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma walipotembelea Halmashauri hiyo.
Mtoza Ushuru Stendi ya wilaya ya Chamwino Hajara Ibrahimu akitoa maelekezo jinsi Mashine za POS zinavyofanya kazi kwa Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma walipotembelea Halmashauri ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chamwino mara baada ya kutembelea Halmashauri ya Chamwino Mkoani Dodoma.
…………………………
Na Alex Sonna-CHAMWINO
MWENYEKITI wa Tume ya Watumishi wa Umma ,Jaji Mstaafu Hamisa Kalombola, amewataka watumishi wa Umma kutunza Siri za Serikali ili kulinda Maslahi ya Nchi.
Hayo ameyasema wakati wa ziara ya Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma walipotembelea Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Jaji Mstaafu Mhe. Kalombola,amewahimiza watumishi kuwa waminifu katika kulitumikia Taifa kwa kulinda maslahi kwa kutunza viapo vyao na kuacha kuvunjisha siri za utumishi.
”Kuna baadhi ya watumishi wa Serikali wamekuwa na mmomonyoko wa maadili kwa kuvunjisha siri za Serikali hivyo tunawaomba waache tabia hiyo walinde viapo vyao kwa kusimamia maadili ya utumishi wao.”amesema Jaji Mstaafu Mhe. Kalombola
Aidha Jaji Mstaafu Mhe. Kalombola amewataka watumishi kuwa wabunifu katika kazi zao ili kuongeza mapato na kujiletea maendeleo kwenye Taasisi zao na wachukulie changamoto kama sehemu ya kazi zao.
Vilevile Jaji Mstaafu Mhe. Kalombola ameeleza kuwa Tume hiyo katika majukumu yake imejiwekea utaratibu wa kutembelea Taasisi pamoja na maeneo mbalimbali ya Serikali kwa lengo la kuelimisha,kuelekeza uwajibikaji na kubadilishana uzoefu ili kuboresha uendeshaji wa usimamizi na maswala ya utumishi kwa mujibu wa sheria.
“Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani inawathamini sana watumishi wa Umma Kwa Mchango mnaoutoa katika kuwahudumia wananchi kwenye kuleta maendeleo yao”amefafanua Jaji Mstaafu Mhe. Hamisa
Kwa Upande wake Kamishna wa Tume, Mhe. Nassor Mnambila amewashukuru viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino kwa muitikio wao na mapokezi yao makubwa kwenye ziara hiyo yenye lengo la kutoa mrejesho na kujifunza namna ya ukusanyaji wa mapato.
“Tunawashukuru viongozi wa Halmashauri hii kwa mapokezi yenu na kukubali kuja kwenu kujifunza namna mashine hizi za posi zinavyotumika kukusanya mapato lakini pia tuwapongeze kwa ujenzi wa madarasa Matatu mukishirikiana na wananchi”. Amesema Mhe.Mnambila
Katika Ziara ya Makamishna wa Tume katika Halmashauri ya Chamwino ilikuwa na lengo la kujifunza, kuelimisha na kuwakumbusha watumishi wa umma kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma,