Featured Michezo

ARSENAL WA MOTO EPL YAIZAMISHA CHELSEA PALE PALE DARAJANI

Written by mzalendoeditor

TIMU ya Arsenal haikamatiki nchini England baada ya kuizamisha Chelsea bao 1-0 pale pale Stamford Bridge Jijini London mchezo wa Ligi Kuu.

Shujaa wa Arsenal ni beki wake kutoka nchini Brazil Gabriel Magalhães dakika ya 63 akimalizia pasi ya Bukayo Saka.

 
Arsenal inafikisha pointi 34 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ikiizidi pointi mbili Manchester City, wakati Chelsea inabaki na pointi zake 21 nafasi ya saba baada ya wote kucheza mechi 13.

About the author

mzalendoeditor