Featured Michezo

ASTON VILLA YAICHAKAZA MAN UNITED

Written by mzalendoeditor

 Aston Villa wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Villa Park.
Mabao ya Aston Villa ya kocha Unai Emery yamefungwa na Leon Bailey dakika ya saba, Lucas Digne dakika ya 11 na Jacob Ramsey dakika ya 49, akitoka kujifunga dakika ya 45 kuwapatia bao pekee Manchester United.
Kwa ushindi huo, Aston Villa inafikisha pointi 15 katika mchezo wa 14 nafasi ya 13, wakati Manchester United ya kocha Erik ten Hag inabaki na pointi 23 za mechi 13 nafasi ya tano.

About the author

mzalendoeditor