Featured Kitaifa

RAIS SAMIA ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anawapa pole wafiwa wote na majeruhi wa ajali ya ndege iliyotokea Bukoba mkoani Kagera.

Rais Samia pia ametoa salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Albert Chalamaila kufuatia vifo vya watu 19 katika ajali hiyo iliyotokea saa mbili na nusu asubuhi. 

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Ziwa Victoria karibu na uwanja wa ndege wa Bukoba ambapo awali majeruhi 26 waliokolewa na kukimbizwa hospitali ya mkoa kwa ajili ya kupata matibabu.

Wakati huo huo, Rais Samia amewashukuru wakazi wa Kagera kwa ujasiri, ushirikiano na jitihada walizofanya kuwaokoa abiria waliozama na ndege hiyo. 

Rais Samia anawatakia wanafamilia pamoja na Watanzania wote kwa ujumla subra katika kipindi hichi kigumu. 

Mwenyezi Mungu azilaze roho za Marehemu wote mahala pema Peponi. Amin.

About the author

mzalendoeditor