Featured Kitaifa

TEMDO YALETA JAWABU UCHAKATAJI  ZAO LA MUHOGO

Written by mzalendoeditor
Mtambo wa kuteketezea taka za hosipitali uliotengenezwa na TEMDO pamoja na mtambo wa kuchakata mafuta ya Alizeti.
…………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Taasisi ya Uhandisi na Usanifu mitambo(TEMDO) pamoja na kuleta majawabu mbalimbali kwa kutengeneza mitambo inayorahisisha watanzania kufikia Tanzania ya viwanda pamoja na utengenezaji wa vifaa tiba Sasa imekuja na mtambo maalum kwaajili ya kuchakata zao la Muhogo.
Akiongea na waandishi wa habari katika maonesho ya SIDO Kanda ya kaskazini mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Prof. Frederick Kahimba amesema katika kukuza uchumi wa viwanda nchini wamefanikiwa kubuni teknolojia mbalimbali za kisasa ikiwemo mtambo wa kuchakata mihogo kwa muda mfupi lengo ni kupunguza gharama ya uagizaji nje ya nchi.
Prof.Kahimba alisema mtambo huo unachakata mihogo tani 12 na kuweza kupata tani tatu za unga kwa siku moja ambapo lengo la kubuni mtambo huo ni kumrahisishia mzalishaji kuona tija katika uzalishaji wake ambapo wanatarajia kufunga lakini kwa upande wa mtambo huo wilaya Handeni mkoani Tanga kwa kushirikiana na bodi ya mazao mchangayiko.
“Taasisi yetu tumesanifu na sasa tunatengeneza mitambo kwa ajili ya kutengeneza sukari kwa kiwango cha mjasiriamali mdogo na wa kati ambapo mitambo hiyo ina uwezo wa kuchakata tani 200 za muwa wa sukari  kwa siku nakutoa tani 20 ambapo mtu yeyote akiwekeza kwenye mitambo hiyo anauhakika wa kuuza tani 20 za sukari kila siku,”Alisema.
Kwa upade wake Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko wa taasisi hiyo  Dkt Sigisbert Mmasi alisema kuwa uwepo wa teknolojia utaweza kuwarahisishia kaI wakulima  wakati wa usindikaji kwani watalazimika kutumia siku moja pekee tofauti na hapo awali ambapo walikuwa wanantumia siku zaidi ya 10 huku wakitumia nishati ya jua katika ukaushaji.
“Kwa kutumia teknolojia hii mkulima ataweza kuvuna mhogo wake na akaukausha siku hiyo hiyo na akaweza kufungasha unga katika vifungashio tayari kwa matumizi ya nyumbani Mimi nadhani kuwa huyu ni mkombozi mkubwa sana na Sasa tutaweza kutoa thamani halisi ya zao Hilo la mhogo”alisema 
Katika hatua nyingine aliwataka wajasirimali ambao ni wamiliki wa viwanda kuhakikisha kuwa wanatumia uwepo wa taasisi hiyo hasa katika uvumbuzi wa mashine na teknolojia mpya ambazo zote zinalenga kuinua uchumi wa taifa 
Alisema kuwa huwa wanawawezesha wadau wa viwanda kwa kuwapa elimu na namna sahihi ya kutumia mashine kwa ajili ya matumizi mbalimbali ndani ya viwanda.
“Lengo letu ni kuona kuwa sekta hasa ya viwanda inakuwa na mapinduzi makubwa kwa kuwa tuna uwezo mkubwa sana wa kutengeneza vitu ambavyo hapo awali vilikuwa vinazalishwa nje ya nchi Sasa tunazalisha na kubuni kwa umairi mkubwa,niwatake watanzania na wamiliki wa viwanda Sasa kutumia taasisi hii ili tubuni wote kwa pamoja.
Mtambo wa kuteketezea taka za hosipitali uliotengenezwa na TEMDO pamoja na mtambo wa kuchakata mafuta ya Alizeti.
Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Uhandisi na Usanifu mitambo(TEMDO) Prof. Frederick Kahimba akionyesha baadhi ya vifaa tiba vilivyotengenezwa na taasisi hiyo.
Baadhi ya mitambo mingine inayotengezwa na taasisi hiyo

About the author

mzalendoeditor