Featured Michezo

SERENGETI GIRLS KUJIULIZA KWA UFARANSA LEO KOMBE LA DUNIA

Written by mzalendoeditor

Timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 17 (Serengeti Girls) jioni ya  Oktoba 14, 2022 wamefanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wao na Ufaransa utakaochezwa saa 4: 30 jioni  saa za nchini India, Oktoba 15  Uwanja wa Pandit Jawaharlal Nehru jijini Goa.

Baada ya Mazoezi Kocha wa timu Bakari Shime ameeleza kuwa hali ya wachezaji iko vizuri, morali ya kupambana ipo kwa ajili ya taifa.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa ( BMT) ameshuhudia mazoezi hayo na kusema wachezaji wana ari, na mazoezi wamefanya vizuri na wanaoenakana wako tayari kuikabili Ufaransa na baadae mechi dhidi ya Canada.

About the author

mzalendoeditor