Featured Michezo

SIMBA YALALA KWA ARTA SOLAR UWANJA WA UHURU

Written by mzalendoeditor

LICHA ya Kumiliki Mpira kwa asilimia 61 Timu ya Simba imepokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa wageni Arta Solar kutoka nchini Djibouti mchezo wa Kimataifa wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Shujaa wa Arta Solar ni Manuncho Athuman dakika ya 89 akifunga bao safi lililowapa ushindi wageni.

Arta Solar walipoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa mabao 3-0 na Azam FC mchezo uliochezwa uwanja wa Chamazi.

Arta Solar wapo nchini wakiendelea kujifua na mechi za kirafiki kujiandaa na mashindano ya klabu bingwa Afrika ambapo watanzia nyumbani kucheza na Al Merrikh kutoka Sudan

About the author

mzalendoeditor