Featured Kitaifa

JESHI LA MAGEREZA BAADA YA KUIBUKA WASHINDI WA JUMLA MAONYESHO YA 88 KANDA YA KATI HII NDIO MIKAKATI YAO

Written by mzalendoeditor

Baadhi ya mazao mbalimbali yanayolimwa na Jeshi la magereza Mkoani Dodoma.

………………………………

Na Eva Godwin-DODOMA

MRATIBU wa maonyesho kanda ya kati pamoja na Mkuu wa Jeshi la Magereza Msalato Dedan Rwemunana ameeleza mikakati yao baada ya kuibuka washindi wa jumla katika Maonyesho ya nanenane ambapo ushindi huo ulitangazwa Agosti 8, 2022 ikiwa imebeba kauli mbiu isemayo “Agenda 10/30:kilimo ni biashara, shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo, mifugo na Uvuvi”.

Akizungumza na Mzalendo Blog Agosti 10, 2022 katika ofisi za Magereza Jijini Dodoma
Amesema wataendeleza kilimo chenye tija na kuwaonyesha Watu kuwa kilimo ni biashara kutokana na Watu wengi kuwa na fikra potofu na kusema Kilimo ni umaskini.

“Mikakati yetu kwa maonyesho yajayo ni kuendeleza kilimo chenye tija hasa katika Taifa letu na kuendelea kutoa elimu zaidi kwa wakulima wengine ili na wao wanufaike zaidi na kilimo kwasababu sisi tunatumia Teknolojia katika uzalishaji wetu”,amesema

“Tunataka watu watoa fikra zao potofu za kusema kilimo ni umaskini kwasababu kwa sasa biashara ya kilimo ndio inaela kuliko biashara nyingine Nchini, Kwasababu sisi mazao yetu tunauza hadi nje ya Nchi na tunapata faida kubwa na Nchi yetu pia inanufaika tunaviwanda vingi vya kijeshi kwaio tutaendelea kuboresha viwanda vyetu kwaajili pia ya kujiandaa na maonyesho ya jayo”.Amesema Romnana

Ameongezea kwa kusema Taasisi nyingine ambazo pia sio za Kijeshi wala sio za kiserikali kuendelea kuhakikisha kwamba kila Mtu anawajibu na uwezo wa kuzalisha mazao mengi kwaajili ya kuendeleza uchumi wake binafsi pamoja na taifa letu na pia Taifa letu litakuwa na chakula kingi na tutaweza kujiendeleza katika mipango mbalimbali ya kuijenga Nchi yetu.

Naye Mtaalamu wa masuala ya Kilimo na Mifugo katika Jeshi la Magereza Jijini Dodoma Bernard Zebedayo amesema kutokana na agenda ya mwaka huu kuwa kilimo ni biashara wamesema wao kama Jeshi la Magereza wamesema wao kilimo owao ni biashara na wanapata kipato kikubwa zaidi katika kilimo Kilimo

“Jeshi la magereza tunalima mazao mbalimbli kuna mazao yanastawishwa katika kanda ya kati na pia mengine nyanja za juu na mazao yote hayo yakishavunwa yanauzwa tunapata kipato kwaio hii ajenda ilishaanza kutekelezwa na itaendelea kutekelezwa

” Na pia sisi Jeshi la magereza tunajitegemea na magereza wengi wanajishughulisha na kilimo na ndio njia pekee ambayo imetutoa huko tulipotoka na kufika hapa tulipo itoshe kusema tu kilimo ni biashara”.Amesema Zebedayo

About the author

mzalendoeditor