Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Nairobi (UNON), Bi. Zainab Hawa Bangura katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki tarehe 23 Julai 2022 jijini Arusha.
Viongozi hao wamejadili juu ya kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Ofisi ya Umoja wa Mataifa Nairobi katika masuala ya upatikanaji wa fursa za ajira, kuwajengea uwezo wananchi katika maeneo mbalimbali ya utendaji, kukuza lugha ya kiswahili kupitia kitengo cha lugha cha ofisi hiyo na ushirikiano katika masuala ya biashara na ugavi.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda kutika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi Ellen Maduhu akifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Mulamula na Bi. Bangura (hawapo pichani).
Maafisa walioambatana na viongozi hao wakifuatilia mazungumzo.
Sehemu nyingine ya maafisa wakifuatilia mazungumzo.
Mazungumzo yakiendelea.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula pamoja na Bi. Bangura wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe walioambatana nao katika mazungumzo yao.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula pamoja na Bi. Bangura wakiagana baada ya mazungumzo.