Featured Kitaifa

SPIKA DKT.TULIA ATEMBELEA KITUO CHA AFYA MWAKIBETE JIJINI MBEYA 

Written by mzalendoeditor

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amefanya ziara ya kutembelea Kituo cha Afya kilichopo katika kata ya Mwakibete Jijini humo pamoja na kuzungumza na Wananchi wa kata hiyo.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia amewakumbusha Wananchi hao kuhusu umuhimu wa kushiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23, 2022 hapa nchini ili kufanikisha upatikanaji wa takwimu sahihi itakayowezesha Serikali kupeleka maendeleo ya habaka kwa taifa.

“Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ametufanyia mengi na makubwa hapa Jijini sasa tunahitaji maendeleo zaidi hivyo ni lazima Serikali inapotaka kupeleka maendeleo sehemu basi iwe na takwimu sahihi za Wananchi wake. Tutakapohesabiwa na kujulikana idadi yetu itafanikisha maendeleo kuletwa kwa haraka hivyo ni muhimu kushiriki sensa” amesema Dkt. Tulia

About the author

mzalendoeditor