MFUNGWA Demi Minor (27), ambaye miezi michache iliyopita alizusha gumzo kubwa baada ya kuwapa ujauzito wafungwa wenzake katika Gereza la Wanawake la Edna Mahan Correctional Facility lililopo New Jersey nchini Marekani, amehamishwa kutoka gerezani hapo.
Demi amepelekwa kwenye Gereza la Garden State Youth Correctional Facility ambalo linatajwa kuwa na ulinzi zaidi, akiwa ndiye mfungwa pekee wa kike kushikiliwa katika gereza hilo.
Demi ambaye alikuwa mwanaume kabla ya baadaye kubadili jinsia na kuwa mwanamke, amewekwa katika chumba cha peke yake gerezani hapo kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kumlinda dhidi ya wafungwa wa kiume lakini pia kuzuia azije kusababisha madhara zaidi kwenye magereza ya wanawake kwa kuwapa ujauzito wafungwa wenzake.
Chanzo:GlobalĀ