MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandiliwa aliyevaa suti katika akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa Insha wakiwa wamebeba zawadi zao na vyeti wakiwa na watumishi wa Shirika la World Vision |
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandiliwa aliyevaa suti katika akiwa
kwenye picha ya pamoja na washindi wa Insha wakiwa wamebeba zawadi zao
na vyeti wakiwa na watumishi wa Shirika la World Vision
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
MKUU
wa wilaya ya Tanga mkoani Tanga Hashimu Mgandiliwa amelitaka Shirika la
World Vision kuhakikisha linaendelea kuwajengea uwezo mkubwa vijana
walioshindanishwa kwenye usomaji wa Insha na uandishi wa Ishana kuibuka
washindi ili kuwaendeleza vipawa mungu alivyowajalia ili kufika mbali
zaidi kimaendeleo.
Mgandilwa aliyasema hayo wakati wa kilele cha
sherehe za uandishi wa Insha kwa shule za Msingi mkoa wa Tanga
iliyohusisha wilaya nne za mkoa wa Tanga iliyandaliwa na Shirika la
World Vision Tanzania iliyoambatana na utoaji wa zawadi
Alisema
vipaji ambavyo vimepatikana visiishie hapo bali viendelezwe ili viweze
kufika mbali ikiwemo kuhakikisha fedha wanazowapa wazazi zisaidie
kuwaendeleza kimasomo na kununua mahitaji ya shule.
Alisema
Shirika hili limelenga kusaidia jamii na kusaidia kutimiza ndoto za
watoto kusoma vizuri basi ni vyema kujikita zaidi katika kuibua vipawa
na kuviendeleza katika masomo yao ili kufikia ndoto zao na kujikwamua
kiuchumi endapo watahakikisha wanapata elimu bora itakayowasaidia kufika
hadi vyuo vikuu na kupata wandishi wazuri wa Insha.
Aidha
aliwataka watoto waliopata zawadi baada ya kuibuka washindi wa Uwandishi
wa Insha kwamba wazingatie vigezo kabla ya kuhariri kazi zao wazingatie
kuwashindanisha walichokiandika wenyewe badala ya kubadilisha maana na
uhalisia wa mtoto ili kuweza kufanikiwa kupata washindi halisi badala ya
kubadilisha maana na mantiki ya Insha yake.
“Kubadilisha maana
ya uhalisia wa maana ya Insha kunaweza kusababisha mtoto kushindwa
kufanya mwenyewe vizuri na kukosa kujiamini wakati wa kuwasilisha
alichokiandika mwenyewe hivyo zingatieni hilo ili kuweza kupata vipawa
vingi katika maeneo tofauti kwenye Halmashauri zetu.
Pia alisema
watoto hao wanatakiwa kuhakikishiwa wanasoma vizuri na kuwekeza nguvu
katika kusaidia familia zao kwani wengine wanatoka katika familia duni
na kushindwa kutimiza malengo yao hivyo ni vyema kuliona hilo nalo ili
kuhakikisha wanafika mbali zaidi na kupata wandishi wazuri kama
watajengewa misingi imara kutokea wakiwa wadogo hadi kufika chuo kikuu.
Alisema
Shirika linauwezo wakuwasomesha watoto hao hadi kufika vyuo vikuu
nivyema kuhakikisha wanaunga nguvu ya pamoja katika kukuza vipawa hivyo
alivyovitunuku vyeti vya sifa katika viwanja hivi vya Usagara.
Awali
akizungumza wakati wa halfa hiyo Meneja wa Kitengo cha Jinsia na
Uchchemuaji Makao Makuu Shirika la World Vision Tanzania Esther Mongi
alisema wao kama shirika wameanzisha kampeni hiyo tokea mwaka 2017 ya
kupinga mimba za utotoni.
Alisema lakini baada ya kutekeleza
kampeni hiyo wakaona hapana mimba pekee haitoshi changamoto iliyopo
kwenye jamii kuna mimba na ndoa za utotoni hivi sasa wana kampeni yao
jukumu lao sote kupinga mimba za utotoni na ndoa na mwaka huu wamekuja
na zoezi la uandiskiha wa insha kwa mikoa 12 Tanzania.
Aidha
alisema wapo mkoani Tanga kutoa zawadi kwa washindi wa ngazi ya wilaya
za mkoa na wamepata washindi watatu ngazi ya wilaya kwenye wilaya tatu
na katika mkoa wa Tanga leo washindi watatu baada ya hapo mshindi wa
kwanza katarasi yake itapelekwa Tamisemi Dodoma ili kupata mshindi wa
kwanza na pili na tatu.
,Sisi kama Shirika la World Vision
tunaamini kabisa ni jukumu lao wote kupinga mimba za utoto na ndoa iwe
mzazi,mlezi, kiongozi wa dini na serikali kupitia insha tumewajenga
uwezo watoto wameweza kuwa na ujasiri kusoma insha zao mbele ya
wenzao”Alisema
Hata hivyo alisema kupitia zoezi na insha
wamefikia shule 544 na kwa mkoa wa Tanga wamezifikia shule 72 hivyo
wanaamini kwenye mikoa iliyopita wamefanya kazi kwa karibu na waandishi
na elimu hiyo itasamba na wanaamini washindi watakuwa mabalozi wazuri.
Katika
mashindano hayo mshindi wa kwanza ngazi ya wilaya alipata 300,000 na
cheti pamoja na baiskeli,mshindi wa pili 200,000,cheti na
baiskeli,mshindi wa tatu 100,000 cheti na baiskeli ili kuweza kuwasaidia
katika masomo yao.
Hata hivyo washindi kwenye ngazi ya
mkoa,mshindi wa kwanza kutoka wilayaani Korogwe Sarah Juma Mussa alipata
500,000 na cheti,mshindi wa pili 400,000 na cheti huku mshindi akipata
350,000 na cheti.