Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, jana Oktoba 28, 2026, ameshiriki katika kutembelea maonesho wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa tatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa ya Afrika na Urusi uliofanyika Moscow Nchini Urusi.

Matembezo hayo yaliyoongozwa na Rais wa Urusi Vladimir Pitin yana kaulimbiu isemayo Jukwaa la Maendeleo Huru: Suluhisho la Juu la Urusi katika Sekta Muhimu za Kiuchumi na Kijamii “, yanaonesha mafanikio ya nchi hiyo katika maeneo yenye uwezo mkubwa wa ushirikiano na Afrika, zikiwemo sekta za viwanda, kilimo, nishati, usafirishaji, fedha, teknolojia za kidijitali na mawasiliano, huduma ya afya na elimu.